Msanii chipukizi wa Bongo Fleva, Venas John Bebu ‘Bebuz’ amenaswa laivu
akivunja amri ya sita (kuzini) na mwanafunzi wa sekondari ufukweni.
Tukio hilo la aibu lilijiri wiki iliyopita mishale ya saa 8:00 usiku
kwenye Ufukwe wa Coco, Dar ambapo polisi jamii walimnasa jamaa huyo
aliyedaiwa ni swahiba mkubwa wa mwanamuziki, Abdul Sykes ‘Dully Sykes’
ambao hivi karibuni walitoa kibao kipya kijulikanacho kwa jina la
Bunyerobunyero.
Mara baada ya kunaswa, Bebuz alianzisha varangati kubwa lakini polisi
jamii walimtuliza kwa virungu kisha kumfunga pingu na kumtaka atulize
mzuka atoe ushirikiano vinginevyo angeumia.
Kijana huyo alitulia kwa muda lakini alipowaona OFM wakipiga picha,
alilianzisha tena na kutaka kuvunja kamera huku akitamba kuwa alikuwa na
uwezo huo.
Hata hivyo, OFM walikuwa makini kama kawaida yao.
Hata hivyo, OFM walikuwa makini kama kawaida yao.
Ufukwe wa Coco umekuwa ukilalamikiwa kwamba hukutanisha watu wenye
malengo mbalimbali lakini wanaokwenda kwa ajili ya kufanya ufuska usiku
ni wengi hasa siku za wikiendi ambako kunakuwa na burudani ya disko.
Kikosi maalum cha kufichua maovu OFM (Opereshen Fichua Maovu) cha
Global Publishers kilipiga kambi katika ufukwe huo kwa muda wa wiki moja
na kushuhudia maovu yanavyofanyika.
Katika siku za hivi karibu, machangudoa wamekuwa wengi ufukweni hapo
na baadhi yao ni vibaka ambao wamekuwa wakitoka nduki na nguo za wanaume
huku wakisachi na kuchukua kila kitu.
CHANZO:GPL
