Monica Lewinsky.
WASHINGTON, Marekani
BAADA ya miaka 10 kupita toka Monica Lewinsky kuwa katika kashfa ya mapenzi na aliyekuwa rais wa zamani wa Marekani, Bill Clinton sasa ameamua kuvunja ukimya ambao ulikuwa ukisambazwa na baadhi ya mitandao na vyombo vingine vya habari.

Monica alitoa ukimya wake kwa kuanika siri zote katika jarida la
Vanity Fair ambalo limetoka jana na litakuwa mtaani Mei, 13 ambapo
alimuelezea Tyler Clementi, 19 kuwa alijinyonga baada ya kuona video
yake mtandaoni iliyokuwa ikimuonesha akimbusu mwanaume mwingine.
Katika jarida hilo, Lewinsky alisema kuwa yeye na mama yeke wamekuwa
wakighadhirika kwa maneno ambayo yalikuwa yakisambazwa kupitia vyombo
mbalimbali vya habari kuhusiana na kuhusishwa kwa kifo cha Clementi
nakusema kuwa ni aibu na dharau kwa jamii.
Mbali na hiyo Lewinsky alielezea pia kuhusiana na kashfa iliyokuwa
ikimuandama ya kuzushiwa kupewa dola milioni 12 (Sawa na sh. za
Tanzania) kwa kutokusema lolote ambapo alikanusha madai hayo nakusema
kwamba anajuta mpaka leo kwa kile ambacho kimetokea kati yake na rais wa
zamani wa Marekani, Bill Clinton.
Imeandaliwa na Andrew Carlos kwa msaada wa mitandao