MENEJA WA EWURA ALIYEKUFA HOTELINI, AAGWA KWA MAJONZI

Jeneza lenye mwili wa marehemu Julius N. Gashaza.
Mke wa marehemu Gashaza, Mama Baraka (mwenye miwani) akiwa na simanzi nzito.
Mwakilishi kutoka Wizara ya Maji akisaini kitabu cha maombolezo nyumbani kwa marehemu Julius Gashaza, Yombo,Vituka jijini Dar.
Mkurugenzi Mkuu wa Ewura, Felix Ngamlagosi (mwenye koti na shati la bluu (katikati) akijadili jambo na baadhi ya maofisa wake msibani.
Mwenyekiti wa Bodi ya Ewura Saimon Sayole (kushoto) na Felix Ngamlagosi (katikati) wakisikiliza mahubiri ya mchungaji (hawapo pichani).
Mwandishi wa habari  wa Gazeti la Nipashe mwenye koti akibadilishana mawazo na waombolezaji msibani hapo.
Ndugu wa karibu wa marehemu wakiwa katika hali ya simanzi.
Felix Ngamlagosi akiongea na mmoja wa wahandisi wake.
Waombolezaji wakibadilishana mawazo msibani.

MWILI wa Meneja Biashara wa Petroli wa Mamlaka ya Udhibiti wa Nishati na Maji (Ewura), Julius Gashaza umeagwa leo nyumbani kwake Yombo, Vituka jijini Dar es Salaam.

Marehemu alikutwa amekufa hotelini katika mazingira ya kutatanisha muda mfupi baada ya kuwasili jijini Dar es Salaam akitoka Dodoma ambako alikuwa akihojiwa na Kamati ya Bunge la Bajeti akimwakilisha Mkurugenzi Mkuu wa Ewura, Felix Ngamlagosi.

Akiwa msibani hapo, Mkurugenzi Mkuu wa Ewura, Felix Ngamlagosi, amesema kuwa ofisi yake imepoteza kiungo muhimu sana na hajui pengo lake litazibwa na nani.
(PICHA/HABARI: HARUNI SANCHAWA / GPL)


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo