YAH : UPOTOSHWAJI WA TAHADHARI YA HALI YA HEWA KUHUSIANA NA MVUA ZINAZOENDELEA KUNYESHA
Mamlaka ya Hali ya Hewa nchini inapenda kukanusha kuhusiana na
taarifa ya ujumbe mfupi wa simu na katika mitandao ya kijamii wenye
maneno yafuatayo : ‘TMA warning heavy rains of strong easterly winds
100km an hour expected to hit Dar coast from Somalia, Heavy rains 120mm
above sea level expected today and tommorrow. People must avoid Sea and
areas near to Sea should be alert cautioned. Tanzania Meteorological
Agency www.tma.gov.tz’
Mamlaka inapenda kuutaarifu umma kuwa
taarifa hiyo siyo ya kweli na ina lengo la kupotosha umma na wala
haijatolewa na Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania.
Mamlaka ina kuwakumbusha wananchi
wote kuendelea kufuatilia taarifa zetu kupitia vyanzo husika vya Mamlaka
vikiwemo utabiri wa kila siku utolewao kupitia radio, televisheni na
tovuti ya Mamlaka (www.meteo.go.tz).
Taarifa sahihi za mwenendo wa
mvua na tahadhari za hali mbaya ya hewa zinatolewa na zinapatikana
kupitia njia rasmi za utoaji taarifa maalum za kiofisi (official weather
statement).
Hivyo taarifa kuhusiana na mvua
zinazoendelea imekuwa ikitolewa katika utabiri wa kila siku kupitia
vyombo vya habari, mtandao wa kijamii wa Mamlaka na tovuti ya Mamlaka.
Tunawatakia shughuli njema katika ujenzi wa Taifa letu.
IMETOLEWA NA MAMLAKA YA HALI YA HEWA TANZANIA
