- Awataka wananchi kutokubali kuyumbishwa
- Awaambia wananchi wa Pemba ,Muungano wa serikali mbili ni rahisi kuusimamia na kuzitatua changamoto zake kuliko wa serikali tatu.
- Asema Viongozi wao wangekuwa wa kweli wangekuwa na makazi ya kudumu na wananchi wao katika kufanikisha maendeleo,badala yake wamekuwa watu wa kuingia na kutoka hivyo kukosa muda wa kusimamia maendeleo ya wananchi.
Katibu Mkuu wa
CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwasili kwenye viwanja vya mkutano
Gombani ya Kale akiongozana na Naibu Katibu Mkuu wa CCM (ZNZ) Ndugu Vuai
Ali Vuai tayari kwa kuhutubia wananchi wa Mikoa miwili ya Pemba.
Naibu Katibu
Mkuu wa CCM (ZNZ) Vuai Ali Vuai akihutubia wananchi wa Pemba kabla ya
kumkaribisha Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana kuhutubia
wananchi wa mikoa miwili ya Pemba katika viwanja vya Gombani ya Kale.
Katibu Mkuu wa
CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wananchi wa Mikoa miwili ya
Pemba na kuwataka kuwa makini na viongozi wenye kauli mbili mbili kwani
hawana nia njema na maendeleo yao zaidi ya kujifikiria wao binafsi.
Katibu wa NEC
Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akihutubia wananchi kwenye viwanja vya
mikutano vya Gombani ya Kale,Pemba na kuwaambia wananchi hao kuwa CCM
itaenda sambamba na wapotoshaji wa ukweli.
Wananchi
wakionyesha ishara ya muundo wa Serikali mbili kwenye mkutano wa hadhara
uliofanyika kwenye viwanja vya Gombani ya Kale,Pemba.
Katibu Mkuu wa
CCM Ndugu Abdulrahman Kinana pamoja na Katibu wa Itikadi na Uenezi Nape
Nnauye na Naibu Katibu Mkuu wa UVCCM Ndugu Shaka Hamdu Shaka na Viongozi
wengine wa CCM Zanzibar wakionyesha ishara ya muundo wa Serikali mbili
za Muungano wakati wa mkutano wa hadhara uliofanyika Gombani ya Kale.
Mabinti wa UVCCM
Pemba wakisoma utenzi wa kumkaribisha KatibuMkuu wa CCM Ndugu
Abdulrahman Kinana kutoka kushoto ni Fatuma Juma Ramadhani na Halima
Juma Haji kwenye viwanja vya Gombani ya Kale.
Sheikh Hamisi
Ali Hamisi akisoma dua kabla ya kuanza kwa mkutano wa hadhara kwenye
viwanja vya Gombani ya Kale Pemba ambapo Katibu Mkuu wa CCM Ndugu
Abdulrahman Kinana alihutubia umati.
Naibu Katibu
Mkuu wa UVCCM Ndugu Shaka Hamdu Shaka akihutubia wakazi wa Pemba na
kuwaambia wawe makini na viongozi wanafiki wa kisiasa.
Makamu Mwenyekiti
wa UWT Bi. Asha Bakari Makame akihutubia wananchi wa mikoa miwili ya
Pemba na kuwaambia kuwa wananchi wawe makini na viongozi wanaotaka
kuvuruga Muungano wetu.









