JAMAA ASHUSHIWA KICHAPO KIKALI BAADA YA KUVAMIA MKUTANO WA UKAWA MKOANI MOROGORO


Njemba huyo akipokea kichapo kutoka kwa wafuasi wa Ukawa mkoani Morogoro na baadaye kuokolewa na polisi.
Mwenyekiti wa Bavicha, John Heche akithibitisha kumtambua kijana huyo anayedaiwa kushiriki kumteka mbunge wao kwenye uchaguzi mdogo uliofanyika Jimbo la Kalenga, lringa.
Mmoja wa viongozi wa Chadema mkoa wa Morogoro, lnnocent Zawadi ambaye alikuwepo jimboni Kalenga naye akithibitihsa pia kumtambua kijana huyo.

NJEMBA mmoja amepokea kipigo kikali kutoka kwa wafuasi wa Ukawa waliokuwa na mkutano mkoani Morogoro jioni hii baada ya kudaiwa kuwa miongoni mwa waliomteka Mbunge Rose Kamli wakati wa uchaguzi mdogo jimboni Kalenga, mkoani Iringa.

Njemba huyo ambaye hakufahamika jina lake mara moja, aliangushiwa kipigo baada ya kuibuka na kuanza kumpiga picha Mwenyekiti wa Bavicha Taifa, John Heche. Baada ya kipigo cha nguvu, njemba huyo alinusuriwa na polisi waliomchukua kumtoa mikononi mwa wafuasi hao.

Mwenyekiti huyo wa Bavicha akithibitisha kumtambua kijana huyo anayedaiwa kushiriki kumteka mbunge wao kwenye uchaguzi mdogo uliofanyika Jimbo la Kalenga, lringa.
(PICHA NA DUSTAN SHEKIDELE / GPL, MOROGORO)


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo