Wanafunzi
wa darasa la tatu na darasa la nne katika shule ya msingi majengo
wakifanya mtihani chini katika uwanja wa shule hiyo mapema leo asubuhi.
Katika
kufikia malengo ya Mpango wa matokeo makubwa sasa katika Sekta ya
Elimu nchini,uongozi wa shule ya msingi majengo wilayani Kahama mkoani
Shinyanga umeanzisha mbinu mpya ya ufanyaji mitihani kwa wanafunzi wao
mbinu ambayo imepokelewa kwa mtazamo tofauti na baadhi ya wazazi wenye
watoto katika shule hiyo.
Licha
ya kuwa shule hiyo ina madawati ya kutosha uongozi wa shule hiyo
umeanzisha mbinu hiyo mpya ambapo wanafunzi wanafanya mitihani yao
wakiwa wamekaa chini katika uwanjani wa shule hiyo bila madawati huku wakiwa umbali wa mita mbili kila mmoja na kuandikia kwenye magoti na chini ya mchanga.
farajimfinanga.com
ilifika katika shule hiyo na kuwakuta wanafunzi wa darasa la tatu na
la nne wakifanya mtihani wa kufunga muhula wa kwanza chini ya vivuli
vya miti katikati ya uwanja wa shule hiyo majira ya saa mbili asubuhi.
Mwalimu mkuu wa shule hiyo William Ngulu alipotafutwa
ili kutoa ufafanuzi wa sababu ya wanafunzi kufanya mitihani chini
licha ya kuwa shule hiyo ina madawati ya kutosha alisema kuwa hiyo ni
mbinu ya kuwafanya wanafunzi wake wafanye mitihani kwa akili binafsi
bila kuangaliziana.
Ngulu
ameongeza kuwa mitihani hiyo hufanyika mida ya asubuhi tu wakati jua
likiwa halijawa kali na kwamba hali hiyo inaleta mafanikio makubwa
katika shule yake katika kufikia mpango wa matokeo makubwa sasa (BRN) BIG RESULT NOW.
>>>>farajimfinanga.com
Katika
hatua nyingine Mwl Ngulu amesema kuwa mbinu hiyo wameanza kuitumia
toka mwaka 2013 na ndiyo siri ya mafanikio ya shule hiyo kuwa ya kwanza
kiwilaya katika matokeo ya darasa la saba mwaka 2013.
Naye mwenyekiti wa mtaa wa majengo ambaye ni mzazi katika shule hiyo Noel Mseveni amesema
kuwa swala hilo si jema na kwamba Kitendo hicho ni kuwazalilisha
watoto na wazazi na kutoa mbinu mbadala ambapo ameshauri wanafunzi hao
wafanye mitihani kwa awamu mbili za asubuhi na jioni ili kuwapa fursa
wote wafanye mitihani wakiwa wameketi kwenye madawati.
Kwa upande wake Afisa elimu msingi katika halmashauri ya mji wa Kahama Aluko Lukolela Aluko amesema kuwa mbinu hiyo ameianzisaha yeye alipohamia wilayani hapo na kwamba imeleta mafanikio makubwa katika kuinua elimu.
Sambamba
na hayo Aluko amepinga mbinu mbadala iliyotolewa na Mwenyekiti wa mtaa
huo na kusema kuwa mbinu hiyo itasababisha kuvujisha mitihani hiyo
kwani wanafunzi watakaofanya asubuhi watakuwa na nafasi kubwa ya
kuwaambia maswali wenzao watakaoingia jioni.
Mbinu
hiyo mpya iliyoanzishwa mjini kahama katika kuhakikisha wanafunzi
wanafanya mitihani kwa akili zao wenyewe bila kuibiana majibu,inamfanya
mkuu wa shule ya msingi majengo Mwl William ngulu kusema kuwa katika mwaka huu 2014 shule yake itaongoza tena ma kuwa ya kwanza kiwilaya katika shule za msingi za serikali.MSIKILIZE MWALIMU MKUU HAPA CHINI
