Zoezi la kuwaondoa ombaomba katikati ya jiji la Dar es Salaam limeanza ambapo halmashauri ya manispaa ya temeke imefanikiwa kuwakamata baadhi ya ombaomba walioonekana katika maeneo ya manispaa yao kwa lengo la kuwafikisha mahakamani na wengine kurejeshwa makwao.
Zoezi hilo limeendeshwa na maafisa wa manispaa ya
Temeke kwa kuzungunguka katika maeneo mbalimbali ya manispaa hiyo kwa
kushirikiana na askari wa jiji na kufanikiwa kuwakamata baadhi ya
ombaomba ambao wanatumia njia ya kuwatuma watoto kuomba pembezoni mwa
barabara,hali ambayo ni hatari huku wakiongeza kuwa zoezi hili si nguvu
ya soda bali ni endelevu