Spika Mstaafu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Pius Msekwa (kulia) akitoa ufafanuzi leo mjini Dodoma kuhusu hati ya Muungano kwa wajumbe wa Kamati namba mbili(2) ya Bunge Maalum la Katiba baada
ya wajumbe hao kumuomba aende kuwaelimisha juu ya hati hiyo. Wengine ni
Mwenyekiti wa Kamati namba mbili Shamsi Vuai Nahodha(katikati) na
Mwanasheri Mkuu wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Othaman Masoud
Othaman(kulia).
Mwanasheri Mkuu wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Othaman Masoud Othaman(kulia) akitoa ufafanuzi leo mjini Dodoma kuhusu hati ya Muungano kwa wajumbe wa Kamati namba mbili(2) ya Bunge Maalum la Katiba baada
ya wajumbe hao kumuomba aende kuwaelimisha juu ya hati hiyo. Wengine ni
Mwenyekiti wa Kamati namba mbili Shamsi Vuai Nahodha(katikati) Spika
Mstaafu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Pius Msekwa (kulia).
Wajumbe
wa Kamati namba mbili wakimsikiliza Spika Mstaafu wa Bunge la Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania Pius Msekwa (hayupo pichani) wakati anatoa
ufafanuzi leo mjini Dodoma kuhusu hati ya Muungano baada ya wajumbe hao kumuomba aende kuwaelimisha juu ya hati hiyo.
Mjumbe
wa Bunge Maalum la Katiba Ali Mzee Ali (kushoto) akiwafafanulia wajumbe
wenzake Kamati namba mbili leo mjini Dodoma kuhusu wazee walioshuhudia
utiaji wa saini hati ya Muungano kwa upande wa Bara na Visiwani. Kulia
ni Mjumbe mwezie Asha Bakari Makame.
Mwenyekiti wa Bunge Maalum
la Katiba Samuel Sitta(kulia) akizungumza na wajumbe wa Kamati namba
Sita (6) ya Bunge hilo leo mjini Dodoma wakati akitembelea Kamati
mbalimbali kujionea maendeleo ya uchambuzi wa vifungu mbalimbali vya
rasimu ya Katiba mpya kwa sura ya Kwanza na Sita. Wengine ni Mwenyekiti
wa Kamati hiyo Stephen Massato Wassira(katikati) na Makamu Mwenyekiti wa
Kamati hiyo Dkt. Maua Abeid Daftari(kushoto).Picha na Bunge la Maalum la Katiba.