Mwenyekiti
wa mkutano wa wazazi/walezi wa shule sekondari kata ya Unyahati jimbo
la Singida mashariki na diwani wa kata hiyo, Abel Richard Suri, (wa pili
kushoto) akisisitiza jambo kwenye huo uliofanyika kwenye viwanja vya
shule ya sekondari Unyahati.Wa kwanza kushoto ni mkuu wa shule ya
Unyahati sekondari, Mkhai Marco.
.ni wanachama wa CCM na Chadema wazika rasmi sera ya kutochangia maendeleo
.iiasisiwa na Mbunge wa Singida mashariki, Tundu Lissu
Na Nathaniel Limu, Ikungi
WANACHAMA
wa CHADEMA na CCM kata ya Unyahati jimbo la Singida mashariki kwa
pamoja wameazimia ‘kuzika rasmi’ sera ya wananchi kugoma kuchangia
miradi ya maendeleo kwa madai kwamba inarudisha nyuma maendeleo ya kata
hiyo.
Sera hiyo inadaiwa kuasisiwa na Bunge (CHADEMA) wa jimbo hilo la Singida Mashariki, Tundu Lissu.
Akizungumza
kwenye mkutano wa hadhara uliohudhuriwa na wanaCCM, CHADEMA na wakazi
wengine wa kata hiyo wapatao zaidi ya 150, Diwani kwa kata hiyo, Abel
Suri amesema sera ya kugoma kuchangia maendeleo ikiwemo sekta ya elimu
imedumaza kwa kiasi kikubwa maendeleo ya kata hiyo.
Akitoa
mfano hai,amesema kuwa kuanzia mwaka 2011 hadi sasa, zaidi ya
shilingi 75 milioni zilizotengwa kwa ajili ya ujenzi wa nyumba za kuishi
walimu wa sekondari ya Unyahati, hazikutolewa kwa sababu wananchi
wamegoma kuchangia na kushiriki ujenzi wake.
Mjumbe
wa mkutano wa wazazi/walezi wa wanafunzi wa shule ya sekondari Unyahati
jimbo la Singida mashariki, akishiriki kujadili mada/changamoto
zinazoikabili shule hiyo, ikiwemo ya uhaba mkubwa wa vyoo.
“Vivyo
hivyo kwa upande wa ujenzi wa maabara tatu, hali ni mbaya zaidi
tumekuwa tukitengewa zaidi ya shilingi 210 milioni, lakini hatuzipati
kwa sababu tumeshindwa kukidhi vigezo ambavyo vinavyohitajika ambavyo ni
kujenga boma la vyumba hivyo”,amesema kwa masikitiko.
Suri
amesema fedha zinazotengwa na serikali kwa maendeleo ya jimbo la
Singida mashariki zote zimekuwa zikipelekwa jimbo la Singida kaskazini
ambako wananchi wake wanachangia na kushiriki kikamilifu utekelezaji wa
miradi yao ya maendeleo.
“Tumekubali
kudanganywa tumeiachia serikali itufanyie kila kitu nadhani kila mmoja
wetu ni shuhuda mzuri kwamba serikali haina uwezo huo tumedanganyika na
sasa tunashuhudia kudumaa kwa maendeleo ya kata yetu”,amesema.
Baadhi
ya wazazi/walezi wa shule ya sekondari Unyahati jimbo la Singida
mashariki,wakifuatilia majadiliano juu ya changamoto zinazoikabili shule
hiyo.
Akifafanua
zaidi, amesema mfano hai ni shule ya sekondari ya Unyahati ambayo
inakabiliwa na changamoto nyingi, ikiwemo ya uhaba mkubwa wa vyoo na
nyumba za kuishi walimu.
“Hivi
sasa wakija maafisa afya,shule hii inafungwa. Shule haina jengo la
utawala inatumia vyumba za madarasa kuwa ni ofisi za walimu haina nyumba
hata moja ya kuishi walimu, walimu wote wamepanga Ikungi kitendo
kinachosababisha watembee kilomita nane kwenda na kurudi
shuleni”,amesema.
Baada
ya maneno hayo, wazazi/walezi kwa kauli moja walikubaliana kufufua moyo
uliokuwepo na kuchangia maendeleo yao na kwa kuanzia wataanza na
kuchangia na kushiriki ujenzi wa vyoo vya shule yao na kisha baadaye
wajenge nyumba za kutosha walimu kuishi katika maeneo ya kituo chao cha
kazi.
Kaimu
mkuu wa shule ya sekondari ya Unyahati jimbo la Singida mashariki,
Mboya David, akikagua choo cha nyasi kinachotumiwa na wanafunzi wa shule
hiyo.Imedaiwa wanafunzi wengine hujisaidia vichakani kitendo
kinachohatarisha maisha yao kutokana kuwepo na nyoka wengi.(Picha na
Nathaniel Limu)