Na Gasper Andrew, Singida.
SERIKALI
na Asasi zake zimeshauriwa kujenga utamaduni wa kuendeleza miradi ya
maendeleo inayoanzishwa na wahisani wa maendeleo ili pamoja na mambo
mengine kuifanya miradi hiy ya wananchi kuwa endelevu.
Imedaiwa
miradi mingi ya maendeleo ya wananchi inayoanzishwa na wahisani wa
maendeleo kufa baada ya kukabidhiwa wananchi na serikali,
Wito
huo umetolewa mwishoni mwa wiki na Mratibu wa Mradi wa ushiriki sawa wa
wanaume katika masuala ya afya ya uzazi na jinsia (TMEP) Mkoa wa
Singida,Mary Sirima wakati akitoa taarifa yake ya maendeleo ya mradi huo
ulioanza mwaka 2010/2011 ambao umepangwa kukamilika desemba mwaka huu.
Amesema
miradi karibu yote inayoanzishwa na wahisani wa maendeleo lengo kuu
huwa ni kuisaidia serikali katika juhudi zake za kuwaondolea wananchi
kero mbalimbali zinazowakabili.
Akifafanua
zaidi, Sirima amesema pamoja na kuwaondolea kero wananchi ipo miradi
mingi tu ambayo inakuwa chachu ya maendeleo katika sehemu husika.
“Kutokana
na ukweli huo upo umuhimu mkubwa kwa serikali na taasisi mbalimbali na
hata watu wenye uchumi mzuri kuchukua hatua ya kuendeleza miradi
inayoanzishwa na wahisani ili iwe endelevu “,amesema Mratibu huyo.
Kuhusu
TMEP, Sirima amesema kuanzishwa kwa mradi huo katika kata 62 za wilaya
ya Singida vijijini na Manyoni wamewafikia watu zaidi ya milioni moja na
kuwapatia elimu ya afya ya uzazi na jinsia.
Amesema
lengo hilo limejikita zaidi kwa upande wa wanaume na msisitizo kwao ni
kwamba wawe chachu ya mabadiliko katika masuala ya afya ya uzazi na
ujinsia.
“Lengo
letu au matarajio yetu ni kwamba tunataka wanaume wajenge utamaduni wa
kuwasindikiza wake zao kliniki na wasione aibu kuwasaidia kufua nguo za
watoto wakiwemo wachanga kupika na kufanya kazi zote za nyumbani, amedai
hatua hii pamoja na faida zake nyingi itaimarisha upendo ndani ya
nyumba”,amefafanua.
Akifafanua
zaidi, Sirima amesema utamaduni uliorithiwa kutoka kwa mababu wa
kuwatumikisha wanawake kama watumwa unachangia kudhoofisha afya za
wanawake kwa hiyo unapaswa kuachwa kwa lengo la kudumisha usawa wa
jinsia.
Mratibu
wa mradi wa ushiriki sawa wa wanaume katika masuala ya afya ya uzazi na
ujinsia (TMEP) mkoa wa Singida, Mary Sirima, akitoa taarifa yake ya
utekelezaji wa mradi huo kwa waandishi wa habari (hawapo kwenye picha).
Baadhi
ya wataribu wa mradi wa ushiriki sawa wa wanaume katika masuala ya afya
ya uzazi na ujinsia (TMEP) waliohudhuria semina ya siku moja ambayo
ilihusu kuwajengea uwezo zaidi wa kutoa elimu kwa jamii.(Picha na
Nathaniel Limu).