Wakazi
wa Kiwangwa, wakivushwa na vijana waliojitolea kujipatia ajira katika
Daraja la Ruvu kwa kuwavusha wananchi kwa kuwabea ama kuwaongoza njia
ili kuvuka eneo hilo la daraja lililojaa maji kutokana na mvua
zinazoendelea kunyesha nchini.
Kamera
ya blog hii iliwashuhudia vijana hao wakiwavusha raia katika eneo hilo
kwa ujira wa Sh. 2000 kwa kila aliyebebwa mgongoni asiyetaka kuvua viatu
ama kugusa maji hayo, na Sh. 500 kwa kushikwa mkono kuongozwa njia
kutoka mwanzo wa maji hayo hadi kuyavuka, na kuyaongoza magari kuvuka
eneo hilo ni Sh. 3000 hadi 5000.
Kutokana na mvua kubwa iliyonyesha jana, Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo, #Ahmed Kipozi,
alifika eneo hilo na kujionea wananchi wakitaabika kuvuka katika eneo
hilo na huku magari ya abiria yaliyokuwa yakitokea Bagamoyo kwenda
Kiwangwa, yakibeba abiria na kuishia eneo hilo na kubeba wengine
walioshushwa upande wa pili na kugeuza kwa kila abiria kulipa Sh. 1000.
Na kisha abiria hao wakipata usafiri mwingine wa kubebwa na Vijana
waliopo eneo hilo kwa Sh. 2000 kwa aliyependa ama 500 kwa kuongozwa
njia.
Vijana
hao wakiliongoza moja ya gari lililokuwa likivuka eneo hilo ambapo
dereva anafuata njia wanayopita vijana hao wa kulia na kushoto hadi
kuvuka ili kuoepuka kupita eneo hatarishi na kutumbukia ama kusukumwa na
maji hayo yaliyokuwa yakionekana kuwa na nguvu kubwa.Mkuu
wa Wilaya ya bagamoyo, Ahmed Kipozi, akizungumza na watendaji wake
aliowaagiza kusimamia zoezi la kuwazuia wananchi kuvuka eneo hilo,
ambapo watendaji hao walimueleza Mkuu huyo wa Wilaya kuwa wananchi
wamekuwa wakaidi na kuamua kukataa kutii amri na kuvuka, jambo
lililomfanya Mkuu wa wilaya kuamua kuagiza askari Polisi wenye silaha
ili kulinda eneo hilo kuwazuia waanchi kuvuka ili kuepuka maafa.
''WA HUKU WA HUKU NA WA HUKO WA HUKO''
Baada
ya hapo Mkuu huyo wa Wilaya alitoa tamko na kuwataka wakazi wa Kiwangwa
kutokwenda Bagamoyo na waBagamoyo kutokwenda Kiwangwa, kwa kipindi
chote cha mvua ili kuepuka maafa yanayoweza kutokea kwa kutumbukia na
kusombwa na maji, ama daraja hilo la Jeshi kukatika kutokana na maji
kuanza kupita juu ya daraja hilo jana.Mkuu
wa Wilaya, akizungumza na madereva wa magari waliokuwa wakisubiri
kuvuka eneo hilo pamoja na vijana waliokuwa wakitoa huduma ya kuwavusha
watu.
Vijana wakifanya kazi yao ya kuwavusha watu eneo hilo.
Baadhi ya magari yaliyokaidi amri yakivuka eneo hilo.Vijana
hao waliwavusha hadi wagonjwa katika eneo hilo kama anavyoonekana
pichani akiwa amembeba mtu mzima anayeonekana kuwa ni mgonjwa.Baadhi ya vijana walijiona kama wapo Beach, walikuwa wakipiga mbizi na kuogelea eneo hilo kwa furaha.Kwa picha zaidi ingia hapa www.sufianimafoto.com