Mgeni rasmi Mwenyekiti wa Chama Cha Msalaba Mwekundu (Red Cross), Dr. George Nangale, akizindu
rasmi kampeni ya ‘Save The Elephant’ (Okoa Tembo) kwa niaba ya Rais
Jakaya Mrisho Kikwete, kama jitihada za kumuunga mkono Rais Kikwete
katika kupambana na ujangili wa wanyamapori nchini. Kushoto ni Mratibu wa Taasisi ya Tembo Marathon Tanzania, Bw. Robert Zangi, Wa
pili kushoto ni Meneja Uhusiano wa Bodi ya Utalii (TTB), Geofrey
Tengeneza, na Kulia ni Dr. Herry Muhando kutoka International
Evangelist.(Picha na Zainul Mzige).
Na. Zainul Mzige.
Taasisi
ya Tembo Marathon Tanzania imezindua kampeni ya ‘Save The Elephant’
(Okoa Tembo) kama jitihada za kumuunga mkono Rais Jakaya Kikwete katika
kupambana na ujangili wa wanyamapori nchini.
Mratibu
wa taasisi hiyo, Robert Zangi, amesema wakati wa uzinduzi wa kampeni
hiyo kwamba wameamua kumuunga mkono Rais Kikwete kutokana na kukithiri
kwa matukio ya ujangili wa wanyamapori miaka ya hivi karibuni. Aliongeza kwamba kampeni hiyo itawalenga zaidi watu ambao wanaishi jirani na mbuga za wanyama.
“Watu wanaoishi jirani na mbuga za wanyama ni rahisi kufahamu nani ni jangili na nani ni raia mwema miongoni mwao,” alisema. Aliongeza
kusema kwamba kampeni hiyo itawafikia watu wanaoishi jirani na mbuga za
wanyama kwa lengo la kuwaelimisha umuhimu wa kupambana na jangili dhidi
ya wanyamapori.
Mratibu
wa Taasisi ya Tembo Marathon Tanzania, Bw. Robert Zangi, akizungumza na
wageni waalikwa wakati wa uzinduzi wa kampeni ya ‘Save The Elephant’
(Okoa Tembo) kupitia Taasisi yake kama jitihada za kumuunga mkono Rais
Jakaya Kikwete katika kupambana na ujangili wa wanyamapori nchini. Wa
pili kushoto ni Meneja Uhusiano wa Bodi ya Utalii (TTB), Geofrey
Tengeneza, Wa pili kulia ni Mgeni rasmi Mwenyekiti wa Chama Cha Msalaba
Mwekundi (Red Cross), Dr. George Nangale (kwa niaba ya Rais Kikwete) na
Kulia ni Dr. Herry Muhando kutoka International Evangelist.
Kampeni
hiyo ina mpango wa miaka mitano ambao kwa kuanzia kutakuwa na matukio
matatu makubwa mwaka huu kati ya sasa hivi na mwezi Mei.
Tukio
la kwanza, alisema, ni la uzinduzi wa kampeni hiyo na la pili ni
kuwasilisha ujumbe wa kampeni kwenye Umoja wa Mataifa nchini Marekani
tarehe 9 mwezi Aprili na la tatu litakuwa ni semina juu ya kupambana na
mauaji ya Tembo, Vifaru na wanyamapori wengine.
Meneja
Biashara wa Qatar Airways Tanzania, Bw. Basel Haydar (kushoto) pamoja
na Meneja Mauzo wa Qatar Airways Tanzania, Bw. Emmanuel Okware.
Meneja
Uhusiano wa Bodi ya Utalii (TTB), Geofrey Tengeneza akisisitiza jambo
ambapo ametoa rai kwa wadau mbalimbali pamoja na mataifa mengine kuunga
mkono jitihadi hizi kuhakikisha ujangili unatokomezwa.
Nae
Mwenyekiti wa Chama Cha Msalaba Mwekundi (Red Cross), Dr George
Nangale, amesema kwamba wanaunga mkono kampeni hiyo kwani mauaji ya
wanyamapori ni majanga na kwamba watu wanaoishi jirani ya mbuga za
wanyama wanaweza kusaidia sana kwenye mapambano dhidi ya ujangili.
Nangale alikuwa anamwakilisha mgeni rasmi ambaye alikuwa awe Rais Kikwete.
Meneja
Uhusiano wa Bodi ya Utalii (TTB), Geofrey Tengeneza, alisema ni vizuri
kuendelea kuwalinda Tembo na wanyamapori wengine na kuongeza kwamba
kampeni hii ni muhimu sana na akaomba jitihada hizi ziungwe mkono na
nchi jirani pamoja na mataifa mengine.