Kumeibuka ongezeko la waganga wa jadi wilayani Makete mkoani Njombe ambao wamekuwa wakijitangaza kwa kuweka mabango yao ya kujinadi katika nguzo za umeme licha ya sheria na kanuni kukataza wao kujitangaza kwa njia hii
Katika pitapita za Eddy Blog tumeshuhudia mabango hayo yakiwa yamesheheni Makete mjini na yamebandikwa katika nguzo za umeme kama unavyoona hii picha hapo juu. Tumeziba namba za simu kwa kuhofia kumtangazia biashara yake na kumuongezea idadi ya wateja. (Picha na Edwin Moshi)
