UCHAFU WAHATARISHA AFYA ZA ABIRIA KITUO CHA MABASI UBUNGO

http://freemedia.co.tz/daima/wp-content/uploads/2014/04/ubt_2.jpg 
BAADHI ya abiria wanaotumia Kituo Kikuu cha Mabasi Ubungo (UBT), wamesema afya zao ziko hatarini kwa kupatwa na magonjwa ya mlipuko kutokana na kusambaa kinyesi kituoni hapo.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti jijini Dar es Salaam jana, abiria hao walisema licha ya Halmashauri ya Jiji kukusanya ushuru kwa madai ya kukiweka kituo hicho katika hali ya mazingira ya usafi, hali ni tofauti.

Walisema kusambaa kwa kinyesi na harufu mbaya ilitokana na kufumuka chemba la majitaka kwa zaidi ya siku tano sasa, huku kukiwa hakuna juhudi zinazofanyika kuondoa kero hiyo.

John Charles, ambaye ni abiria, alisema alishangaa kuwaona watendaji wa jiji kufika katika eneo hilo huku wakishindwa kuchukua hatua za haraka kwa ajili ya kulinda afya za abiria.

“Hali ni mbaya, tumewaona watu wa jiji walikuja na kuangalia kisha wakaondoka bila kufanya 
chochote,” alisema.

Christina Donald, alishauri viongozi wanaohusika  kuangalia kituo hicho na kuchukua hatua za haraka ili kunusuru afya za abiria.

 Tanzania Daima


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo