Hii ndio pick up uliyogongana uso kwa uso la lori na kusababisha vifo vya watu wawili usiku wa leo mjini Iringa
Hili ndilo lori
lililogongana uso kwa uso na pick up eneo la Kibwabwa mjini Iringa
na kusababisha vifo vya watu wawili.
Eneo la ajali
WATU
wawili wamefariki dunia katika ajali mbaya ya pick up kugongana na
lori katika eneo la Kibwabwa barabara kuu ya Iringa - Mbeya usiku
wa kuamkia leo
Kwa
mujibu wa mashuhuda ajali hiyo imesababishwa na dereva wa gari
dogo kuhama upande wake na kulifuata lori hilo kampuni ya Pro-Trans
Ltd ya jijini Dar es Salaam ambalo lilikuwa likitokea barabara ya
Mbeya kuja Iringa na gari hilo dogo lilikuwa likitokea Iringa
mjini.
Akielezea
tukio hilo mmoja kati ya mashuhuda John Sanga alisema kuwa wakati
ajali hiyo ikitokea alikuwa katika kituo cha Mafuta kilichopo eneo
hilo na kushuhudia jinsi ambavyo dereva wa pick up hiyo akilifuata
lori hilo kabla ya kutokea ajali hiyo mbaya .
Hata
hivyo alisema dereva wa gari hilo dogo alionyesha kumfuata dereva
wa lori ambapo dereva huyo ya lori alionyesha jitihada za
kumkwepa bila mafanikio .
Alisema
katika ajali hiyo dereva alikufa papo hapo huku abiria wake
alikimbizwa katika Hospital ya Rufaa ya mkoa wa Iringa na
kufariki wakati akipatiwa matibabu
CHANZO : FRANCIS GODWIN BLOG