Jamaa wa baadhi ya waathiriwa 250 wa ajali ya Ferry nchini Korea Kusini ambao bado hawajapatikana, wamekabiliana na polisi.
Walinzi wa bahari katika pwani ya nchi hiyo, walishindwa kueleza ni sehemu gani hasa ambapo miili hiyo ilipatikana ndani ya ferry hiyo baada ya kushindwa kuona vyema wakiwa chini ya bahari.
Meli hiyo ilizama siku ya Jumatatu ikiwa imewabeba watu zaidi ya mia nne wengi wakiwa wanafunzi wa shule.
Mawimbi makali na hali mbaya ya hewa inaathiiri shughuli ya kuwatafuta waathiriwa.
Waendesha mashitaka wanasema kuwa wakati wa ajali hiyo kulikuwa na nahodha mwingine asiye na uzoefu aliyekuwa ameshikilia usukani wa meli hiyo.
Nahodha huyo alikamatwa pamoja na nahodha wa ferry hiyo na wafanyikazi wengine.
chanzo:bbc swahili
