Wananchi
wa kijiji cha Bugulula katika kata ya Bugulula wiayani Geita mkoani
Geita, wamemtaka mwenyekiti wa kijiji hicho Bwana Bahati Matati
kulirudisha shamba lao walilokuwa wakilitumia kwa ajili ya maziko
baada ya kujimilikisha na kuanza kulima mihogo.
Wakiongea
kwa nyakati tofauti jana na waandishi wa habari wananchi hao wamesema
wanashangaa kuona mwenyekiti wa kijiji hicho anachukua shamba hilo
lililotengwa na wananchi kwenye mkutano wa serikali ya kijiji kwa ajili
ya maziko.
Wananchi hao wameongeza kuwa kitendo cha mwenyekiti huyo kupora shamba hilo na kujimilikisha kinyume cha sheria, si cha kiungwana hivyo wameiomba serikali kuweza kulirudisha eneo hilo kwa wananchi ili liendelee na kazi iliyokusudiwa ya maziko.

Kwa
upande wake mwenyekiti huyo Bwana Matati, amesema shamba hilo ni mali
yake na alipewa na uongozi wa serikali ya kijiji baada ya kuingia
madarakani, na kuongeza kuwa hizo ni chuki kwa baadhi ya wananchi.
Wananchi wa kijiji cha Bugulula wamekuwa na madai mengi na ya muda mrefu, kuhusu eneo hilo licha ya kupewa eneo lingine ambalo wanadai lina mawe hivyo hawawezi kuchimba umbali mrefu kwa ajili ya maziko.
Na Valence Robert - Geita