Mtoto
mwenye umri wa miaka (14) ambaye ni mwenyeji wa Rombo mkoani
Kilimanjaro anayeripoti manyanyaso kutoka kwa mtu anayedaiwa kuwa bosi
wake.Mtoto huyo ambaye ni mwenyeji wa Rombo mkoani Kilimanjaro alizama jijini Dar na kuajiriwa katika duka hilo mwanzoni mwa mwezi Novemba, mwajka jana.
Akizungumza na mwanahabari wetu kwa masikitiko, mtoto huyo alisema tangu aajiriwe na mama huyo hajawahi kulala nyumbani bali alikuwa akilala hukohuko kwenye duka ambalo ni dogo halafu limejaa vitu vingi na alikuwa akifungua saa 12:00 asubuhi na kufunga saa 5:00 usiku kila siku.
Akielezea kwa uchungu mateso aliyoyapata tangu afike kwa mama huyo, mtoto alidai alikuwa akipigwa bila sababu na kusingiziwa kuwa ameiba fedha kisha kunyimwa chakula.
Kwa mujibu wa mtoto huyo, kuna mama mmoja jirani yao aliyekuwa akishuhudia mateso yake hivyo akawatafuta wanaharakati wa haki za binadamu ambao walichunguza ishu na wakajiridhisha kweli mtoto huyo alikuwa akinyanyaswa. Akizungumza na gazeti hili, mmoja wa wanaharakati hao alisema kwa kuwa walishatoa elimu mitaani na kama yakitokea masuala kama hayo basi wananchi wawasiliane nao.
Mwanaharakati huyo alisema kuwa walipigiwa simu wiki mbili zilizopita kuwa kuna mtoto anateswa ndipo walipofanya uchunguzi katika eneo alilokuwa akifanyia kazi.
Wanaharakati hao waliwasiliana na polisi wa Kituo cha Oysterbay, Kinondoni, Dar ambapo mama huyo alikamatwa na kufunguliwa jalada la kesi namba OB/RB/5205/2014 UNYANYASAJI WA MTOTO huku akisubiri kufikishwa kwa kortini.
CREDITS:GPL