Moto
umeteketeza vibanda vya biashara viwili mali ya Bw.Edson Tweve na
Denyelela Mahenge katika kijiji cha Isapulano Kata ya Isapulano wilayani
Makete Mkoani Njombe usiku wa kuamkia leo mnamo saa 6 usiku hadi saa 9
Usiku
Kwa
mujibu wa mtoa taarifa wetu Bw. Kumbusho Mhenge kutoka katika kijiji
hicho amesema "Tukio hilo linasemekana kuhusika na Mtu/watu
wasiojulikana usiku wa kuamkia leo katika kijiji hicho ambapo mashuhuda
wa tukio wameelezea jinsi walivyoshuhudia kuwa Kibanda kimoja cha
Bw.Edson Tweve kilibomolewa na kumwagiwa Mafuta aina ya Petrol na
kuwashwa moto ambapo ulipamba katika chumba cha jirani na moto kuendelea
kurindima"
"Niligundua
kuwaka kwa moto huo mnamo saa 6 hivi usiku katika kibanda changu lakini
sikuwa na hofu zaidi kwani nilijua huenda ni moshi wa kawaida, lakini
ilipofika saa 9 usiku nikamwamsha mume wangu ndipo tulianza safari za
kuelekea hapo tukakuta kibanda kimeteketea chote kwa moto na kuanza
kupiga mayowe kwa majirani"Alisema Mke wa Bw.Edson
Hata
hivyo taarifa ilitolewa katika kituo cha Polisi ambapo walifika katika
eneo la tukio lakini hakuna mtu yeyote aliyekamatwa wala kuhisiwa na
tukio hilo hadi sasa
"Uongozi
wa kijiji nao umesema kuwa tukio hilo ni la kusikitisha na kutishia
amani iliyopo kijijini hapa na kila mmoja wetu ni vema akawa Mpelelezi
ili kufanikisha kuwakamata wahalifu hao"Alisema Bw.Kumbusho Mhenge
Msomaji wa Mtandao huu tutaendelea kukujulisha kwa kadri tutakavyokuwa tunazipata habari hizi kwa Undani zaidi
Na Furahisha Nundu