MMOJA AFARIKI DUNIA KWA AJALI YA PIKIPIKI,NA MWINGINE AKAMATWA KWA KUUZA BHANGI MKOANI NJOMBE

Na Gabriel Kilamlya, Njombe
Jeshi la Polisi Mkoani Njombe Limethibitisha Kutokea Kwa Matukio Mawili Tofauti Likiwemo la Ajali Ya Barabarani na Kusababisha Kifo Cha Mkazi Mmoja wa Ikelu Wilayani Njombe.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Njombe SACP Fulgence Ngonyani Amesema Kuwa Tukio la Kwanza Limehusisha Ajali ya Waendesha Pikipiki Ambapo Aprili 19 Mwaka Huu Majira Ya Saa Nane Usiku Huko Katika Maeneo Ya Ilunda Kata Ya Mtwango Wilayani Njombe Katika Barabara Ya Njombe-Makambako Pikipiki Yenye Namba za Usajili T.570 BML Aina ya SANLG Ikiendeshwa na Batista Gadau Mwenye Umri wa Miaka 38 Ambaye ni Mkazi wa Lyamkena Makambako Iligongana  na Pikipiki Yenye Namba za Usajili T.326 CLB Aina ya TOYO Iliyokuwa Ikiendeshwa na Cryford Matandala na Kusababisha Kifo cha Dereva wa Pikipiki Hiyo.

Aidha Kamanda Ngonyani Amesema Ametoa Wito Kwa Wananchi Juu ya Kuendesha Vyombo Vyao Vya Moto Kwa Kuzingatia Sheria za Usalama Barabarani.

Katika Tukio la Pili Kamanda Ngonyani Amesema Kuwa Jeshi la Polisi Linamshikilia Ibrahim Abdi Mwenye Umri wa Miaka 37 Mkazi wa
National Housing Mjini Njombe Kwa Tuhuma za Kukutwa na Madawa Ya Kulevya Aina Ya Bhangi.

Kamanda Ngonyani Amesema Kuwa Tukio Hilo Limetokea Aprili 18 Mwaka Huu Majira Ya Saa 03:00 Usiku Ambapo Mtuhumiwa Huyo Alikutwa na Madawa Hayo Ya Kulevya Aina Ya Bhangi Kete Mbili na Rizra Pakti Moja Kwenye Kibanda Anachotumia Kufanyia Biashara Ndogondogo.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo