Nabii Josephat Mwingira.
Katika shauri hilo ambalo ni namba 24 la mwaka 2013, litatajwa Aprili 8, mwaka huu mjini Moshi mbele ya Jaji Ama-Isario Munisi, imedaiwa kuwa mlalamikiwa wa kwanza Dk.
Phils Morris Nyambi na mlalamikiwa wa pili, Nabii Josephat Mwingira ambaye ni kiongozi wa Kanisa la Efatha, wamechukua shamba la hekari 37 la kampuni hiyo lililopo Bomang’ombe, wilayani Hai, mkoani Kilimanjaro bila ridhaa yao.
Profesa Wade Sapp (kulia) anayedaiwa kuwaburuza mahakamani, Nabii Mwingira na Dk. Phils Morris Nyimbi (kushoto).
Hati ya mahakama iliyoandaliwa na Wakili Desidery Ndibalema wa Kampuni ya Bin Attorneys anayemuwakilisha mzungu na kampuni hiyo imesema kwamba Dk. Phils Machi 30, 2007 alilipa kiasi kilichobaki cha shilingi 20,000,000 kwa mwenye shamba baada ya kupewa na mzungu huyo.
Wakili Ndibalema ameeleza kuwa Januari 14, 2009 Dk. Phills bila kuwa na idhini ya Profesa Sapp au kampuni yao, alimpatia shamba hilo mlalamikiwa Nabii Mwingira ambaye anadaiwa kuzaa naye mtoto, kama zawadi (Gift Deed) ambapo aliipa kazi Kampuni ya Geo Land Consult Ltd kupima eneo hilo.
Hata hivyo, mlalamikaji tayari ametuma maombi kwa kamishna wa ardhi wa Moshi ili eneo hilo lipimwe kwa nia ya kujenga hospitali, ofisi ya mazingira na hoteli ya nyota tano ili kuwa kumbukumbu ya Dk.
Betty Sapp (alifia Moshi kwa ajali miaka ya nyuma), ambaye alikuwa mke wa Profesa Sapp anayetarajia kuja kutoa ushahidi wa kesi hiyo.
Mlalamikaji ameiomba mahakama itangaze kuwa Kampuni ya Global 2000 (2010) International na mzungu huyo kuwa ni wamiliki halali wa eneo hilo na kuwaamuru walalamikiwa kulipa gharama ya kesi hiyo na nyingine ambazo mahakama itaona inafaa.
Profesa Sapp alikuwa ni Rais wa Taasisi ya Wanasayansi ya Marekani na sasa amestaafu.
CHANZO:GPL