March 23 2014 lilivamiwa kanisa moja huko Mombasa Kenya watu wakiwa
katikati ya ibada ambapo waliovamia walitekeleza mauaji kwa risasi huku
miongoni mwa waliouwawa akiwa ni mama wa mtoto huyu aitwae Satrin.
Inasemekana mama huyu aliuwawa kwa risasi akiwa kamkinga mwanae
asipatwe na risasi lakini hata hivyo risasi hiyo ilimuua mama na kwenda
kutua na kubaki kwenye kichwa cha mtoto Satrin ambae alikimbizwa
hospitali na siku kadhaa baadae risasi ikatolewa.
Taarifa ya leo kutoka hospitali ya Kenyatta Nairobi Kenya, Satrin
Osinya ameruhusiwa kuondoka hospitalini leo baada ya hali yake kiafya
kuimarika toka alipotolewa risasi kichwani.
Baba yake aitwae Ben Osinya anasema amefurahishwa na hali ya mwanae
ambapo furaha yake ilianza wakati alipopata habari ya kufanikiwa katika
upasuaji ulioitoa risasi.
