Oparesheni Nzito ya kuzuia
Bodaboda na Bajaji zisifanye safari zake kutoka Mwenge na maeneo
mengine kuelekea mjini Posta imechukua sura mpya leo baada ya Askari wa
Usalama wa Barabarani kuanza kukamata Bodaboda na Bajaji zote zinazovuka
Mwenge kuelekea Posta, Zoezi hilo ambalo limefanyika Mwenge Mataa
Jijini Dar limeendelea kufanyika na kufamikiwa kuwanasa wengi.
Kwa mujibu wa Msemaji na
Muongozaji wa Oparesheni hiyo ambaye hakutaka kutajwa jina lake alisema
kwamba wameamua kufanya hivyo ili kuzuia Msongamano wa Magari pamoja na
bodaboda pia Bajaji kuelekea Mjini Posta, Aliongeza kuwa kumekuwa na
uhalifu sana wa Silaha unaotumiwa na bodaboda hasa maeneo ya mjini hivyo
ndio maana wameamua kuzuia.
“Tumefanya hivi ili kuepusha
msongamano kuelekea Posta, lakini pia kumekuwa na uhalifu sana
unaotumiwa kwa njia ya Bodaboda hivyo tunafanya oparesheni hii ili
kupunguza tatizo hili.
Tulicho kifanya tumewaruhusu kufanya safari
pembezoni mwa mji tuu hivyo Eneo la Mwenge kwa sasa Limeingia katika
zone ya eneo la Mjini,Kama tuliweza kuzuia Daladala ndogo”Hiace” pia na
hawa watakuja kuelewa ingawa ni zoezi gumu na linalo hitaji elimu ya
ziada ambayo tumesha anza kuwapa na tunaendelea kuwapa” alimalizia kwa
kusema “Pia hii ni Oparesheni ya kawaida tuu ya kukamata wale ambao
hawana Leseni za kuendesha vyombo hivi pamoja na makosa mbalimbali”
alisema Polisi huyo.
Kwa mujibu wa madereva wa
Bodaboda na Bajaji wamesema kwamba huo ni uonevu kuwakataza wao wasiweze
kwenda Mjini kwani na wao wanatafuta ridhiki yao na wameomba Serikali
iwasaidie wapatiwe njia mbadala ya wao kwenda maeneo hayo.
Wanao ruhusiwa kwenda Posta na
Bajaji au Bodaboda ni wale ambao ni wamiliki binafsi na wanatakiwa
wapite njia hizo wakiwa Bila abiria yoyote.
Askari wa Usalama wa
Barabarani akiwa anawaandikisha Baadhi ya Bodaboda na Bajaji wenye
makosa mbalimbali ili waweze kulipia tozo pamoja na kupelekwa kituo cha
Polisi.

Baadhi ya Bodaboda na Bajaji wakiwa wanangojea Hatma yao baada ya kukamatwa.


Baadhi ya Bodaboda zikiwa zimekamatwa.

Madereva wa Boda Boda na Bajaji wakipata maelezo ya kina ya kwanini wamezuiliwa kwenda Posta wakitokea Mwenge.

Mmoja wa Madereva wa Bodaboda akiwa amekaa kwa mawazo asijue anafanya nini Baada ya Bodaboda yake kukamatwa na Kupelekwa Polisi.(Picha na Dar es salaam yetu).
Baadhi ya Bodaboda na Bajaji wakiwa wanangojea Hatma yao baada ya kukamatwa.
Baadhi ya Bodaboda zikiwa zimekamatwa.
Madereva wa Boda Boda na Bajaji wakipata maelezo ya kina ya kwanini wamezuiliwa kwenda Posta wakitokea Mwenge.
Mmoja wa Madereva wa Bodaboda akiwa amekaa kwa mawazo asijue anafanya nini Baada ya Bodaboda yake kukamatwa na Kupelekwa Polisi.(Picha na Dar es salaam yetu).
