HALMASHAURI YA JIJI LA MBEYA YAKATAA KUPOKEA BARABARA ILIYOJENGWA CHINI YA KIWANGO KATIKATI YA JIJI

HALAMSHAURI ya Jiji la Mbeya imekataa kuipokea Barabara inayoanzia katika Hospitali ya Rufaa ya Meta kwenda katikati ya Jiji yenye urefu wa Kilomita 2.1 baada ya Mkandarasi wa ujenzi wake Kampuni ya China International Construction, CICO kuijenga chini ya kiwango.

Kutokana na hali hiyo Mkandarasi wa ujenzi huo atalazimika kuifumua na kuijenga upya barabara hiyo ambayo ujenzi wake ulikamilika mapema mwaka huu.

Barabara ya Meta kupitia kituo kikuu cha Mabasi cha jiji la Mbeya hadi mjini ni miongoni mwa barabara kongwe zilizojengwa mwishoni mwa miaka ya 1970 na tangu kipindi hicho haikuwahi kufanyiwa matengenezo makubwa zaidi ya haya ya mwishoni mwa mwaka jana.

Kufumuliwa na kujengwa upya kwa barabara hiyo kulikoigharimu serikali kiasi cha shilingi Bilioni 1.4 kupitia mfuko wa Brabara (Road Fund) kuliibua hisia za matuamani kwa watumiaji wake na hasa wenye vyombo vya usafiri lakini matumaini hayo yanayeyuka muda mfupi baada ya ujenzi huo

Wananchi hao wameenda mbali zaidi kwa kuzilaumu mamlaka husika kwa kitendo cha kuyaruhusu magari yenye uzito mkubwa kuingia katikati ya jiji huku zikijuwa kuwa kufanya hivyo kunachangia uharibifu wa barabara.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo