skip to main |
skip to sidebar
D KNOB ATAJA SABABU ZA KUFUNGA NDOA KIMYA KIMYA
Hit maker wa single mpya ya Nishike mkono D knob leo ame-amplify
sababu za kuamua kufunga ndoa ya kimya kimya mwaka 2009 huku idadi ya
watu waliohudhuria pamoja na maharusi wenyewe ikiwa sio zaidi ya 10
kuanzia kanisani mpaka walikoelekea baada ya kutoka kanisani.
Ameongea na millardayo.com na
kusema ‘nilitaka kuifanya na mwenzangu nikamwambia tumekua wapenzi
lakini sasa yahitaji tuwe ndani ya ndoa akasema twenzetu tukaongozana
mpaka kanisani padri akasema hamuwezi kuoana nyie mnajua hata ndoa ni
nini?kuna hatua’
‘Siyo
kitu ambacho tulitaka kufanya kama watu wengi wanavyofanya ile kukaa
kuchangishana kwa sababu mimi rafiki zangu wa karibu wote walikua block
nisingetaka kufunga ndoa halafu mwisho wa siku tuanze kununiana kuwa
huyu hajachanga yule kachanga chapili nilitaka kufanya ili niendelee na
maisha yangu kama mtu unapoamua kufanya birthday’
‘Wazazi walipata taarifa mwishoni kwa sababu hata mzee katika risala
yake maana tulikaa kwenye meza moja baada ya ndoa mzee akasema mimi
sijui nakupa zawadi gani maana umeniambia jana tu,kitu tulichofanikiwa
ni gauni la mke wangu maana ni gauni la gharama nashukuru Mungu lilitupa
stress mwanzo lakini liliwahi’.
millardayo.com
JIUNGE NA EDMO BLOG SASA
Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube
Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi