Mwanadada mkali wa Bongo Movies, Yobnesh Yusuph ‘Batuli’ amefunguka kuwa kwa sasa yupo tayari kuigiza nusu uchi kwa sinema za nje ya nchi.
Akiongea nasi juzi kati, Batuli alisema kuwa muvi nyingi
Bongo huwa zinafungiwa kwa kukosa maadili na kwamba kama ikitokea
nafasi akaitwa nje ya nchi kuigiza sini hizo, atakuwa tayari.
“Zamani
nilikuwa nikiogopa kuigiza nusu uchi. Wenzetu Nigeria wameendelea na
ndiyo maana wanaigiza hata nusu uchi, kama itatokea nafasi ya kuigiza
huko (nje ya Bongo) nusu uchi, nipo tayari,” alisema Batuli.
