BABY MADAHA AJIBU MAPIGO KWA STEVE NYERERE

Stori: Nyemo Chilongani VITA ni vita! Mwanadashosti anayesukuma maisha laifu kupitia filamu na muziki Bongo, Baby Joseph Madaha amesema anamshangaa Mwenyekiti wa Klabu ya Bongo Movie Unity, Steve Mengere ‘Steve Nyerere’ kwa kauli aliyoitoa dhidi yake kuwa hayupo sehemu yoyote ile.

Akifafanua kuhusiana na kauli hiyo aliyoitoa mwenyekiti huyo wiki iliyopita, Baby alijibu mapigo kuwa kiongozi huyo alipotosha umma kwani yeye ni memba halali wa Bongo Movie Unity.
Mwenyekiti wa Klabu ya Bongo Movie Unity, Steve Mengere ‘Steve Nyerere’.

“Steve anasema hajui nipo wapi, hivi ni kweli mwenyekiti hawajui watu waliokuwa na kadi ya uanachama? Mimi nipo kotekote, nipo Bongo Movie, nipo hata Bongo Fleva, kama akitaka kadi aseme nimwoneshe, sionekani sana kwani muda mwingi nakuwa Kenya,” alisema Baby Madaha, alipotafutwa Steve, hakuwa tayari kufafanua ishu hiyo.

GPL


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo