Meli ya Australia ikiwa kwenye zoezi la utafutaji wa ndege ya Malaysia iliyopotea kabla ya zoezi hilo kusitishwa.
IDARA ya usalama wa baharini ya Australia imetangaza kwamba shughuli
za kuitafuta ndege ya abiria ya Malaysia zimesimamishwa kwa muda
kutokana na hali mbaya ya hewa.
Idara hiyo imesema imefanya tathmini na kubainisha kuwa hali mbaya ya
hewa itautatiza uchunguzi unaofanywa kutokea angani na majini na
inaweza kuyahatarisha maisha ya marubani.
Uamuzi huo pia unatokana na tangazo la Waziri Mkuu wa Malaysia, Najib
Razak la kuthibitisha kwamba ndege hiyo iliyokuwa inatafutwa imeangukia
kusini mwa bahari ya Hindi .
Watu 239 walikuwamo katika ndege hiyo iliyotoweka zaidi ya wiki mbili zilizopita.