YANGA WAPATA AJALI MIKESE MOROGORO, BASI LAO LATUMBUKIA MTARONI

Basi la timu ya Young Africans lililokuwa limebeba wachezaji pamoja na viongozi wa benchi la ufundi limepata ajali eneo na Mikese Mizani mkoani Morogoro baada ya Mabasi yaliyokua yakitanua kuelekea mikoa ya bara kuziba njia na kusababisha kutumbukia kwenye mtaro.

Basi hilo limepata ajali likitokea mkoani Morogoro kwenda Dar es Salaam baada ya mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Mtibwa Sugar uliopigwa kwenye Uwanja wa Jamhuri, Morogoro jana.

Taarifa zinasema Katika ajali hiyo iliyotokea majira ya saa tatu na nusu asubuhi hakuna mtu yeyote aliyejeruhiwa na kwa sasa timu inaondoka na usafiri wa basi jingine kuelekea jijini Dar es salaam.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo