Watoto hao walipokuwa wamelala na kuteketea kwa moto ambao chanzo chake inadhaniwa kuwa ni hitilafu za umeme.
 |
Miili
ya watoto wawili wa familia moja Daniel Paul(8)na mdogo wake Emmanuel
Paul(3) ambao wamepoteza maisha baada ya nyumba waliokuwa wakiishi
kuteketea kwa moto huku wakiwa wamelala ndani majira ya saa moja asubuhi
peke yao huko eneo la mtaa wa Rufita Mwanza road Tabora mjini.
 |
Kamanda
wa Polisi wilaya ya Tabora OCD Samwel Mwampashe akizungumza na
wananchi wakati wa tukio hilo la kusikitisha lililotokea na kupoteza
maisha ya watoto hao. |
 |
Katikati
alijishika kichwani ni Paul Daniel ambaye baba wa watoto hao
walipoteza maisha akiangalia maiti za watoto wake hao wawili muda mfupi
mara baada ya kufika eneo la tukio ambapo maswali mengi yalizuka baba
huyo alikuwa wapi wakati watoto wanateketea kwa moto ndani ya nyumba. |
 |
Mkuu
wa wilaya ya Tabora Bw.Suleiman Kumchaya alifika eneo la tukio mapema
wakati Kikosi cha Zimamoto kikimalizia uzimaji wa moto na kuwatoa
watoto hao ambao tayari walikuwa wamekwisha kufa. |
 |
Huyu mama na mtoto walisalimika katika tukio hilo la moto ambao walikuwa kwenye vyumba vingine |
 |
Baadhi ya Samani ziliteketea vibaya kwa moto huo. PICHA ZOTE KWA HISANI YA KAPIPIJ BLOG |
|
|