Mratibu
wa Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu (THRDC), Ndg. Onesmo
Olengurumwa akitoa mada juu ya ya mtazamo na jukumu la wabunge wa katiba
na waandishi wa habari za katiba pamoja na watetezi wa haki za binadamu
katika mchakato wa kuandika Katiba mpya mkutano wa siku moja
uliofanyika mjini Dodoma.
-Waambiwa waache kamari ya majongoo kuhusu serikali mbili ama tatu
-Watetezi wa haki za binadamu, waandishi watoswa kwenye rasimu ya Katiba
Na Damas Makangale, Dodoma, MOblog
WAANDISHI na Wahariri wa vyombo vya habari nchini wamehimizwa
kuzingatia maadili ya uandishi wa habari na kuweka mbele maslahi ya
taifa wakati wa kuripoti Bunge maalum la katiba. MOblog inaripoti.
Akifungua warsha ya siku moja kwa waandishi wa habari kuhusu nafasi
ya watetezi wa haki za binadamu na asasi za kirai katika katiba mpya
jijini Dodoma, Makamu Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba, Mhe Samia
Sululu Hassan amesema waandishi wa habari wana nafasi kubwa ya
kuelimisha jamii juu ya haki za binadamu kupitia kalamu zao kwa
kuzingatia weledi wa fani yao na maadili ya uandishi.
“waandishi wa habari pamoja na wahariri wao wanaweza kwa kuweka mbele
maslahi ya taifa kuripoti na kuandika habari zenye kuleta suluhu,
amani, mshikamano na utulivu,” amesema.
Amesema waandishi wa habari kwa kutumia
kalamu zao wanaweza kushauri na kushirikiana na serikali na mamlaka
zingine kupatikana kwa katiba mpya yenye tunu za taifa,
Sululu aliongeza kwa kuweka hoja zao kwa
ari ya utulivu wanaweza kabisa kuleta mshikamano na ushirikiano wa
kitaifa katika kudumisha amani na haki za binadamu nchini.
Amesema kwamba kupitia bunge la katiba
wanahabari ni kiungo muhimu katika kufikisha ujumbe kwa wananchi na
kuelimisha umma jinsi sheria na haki za binadamu zinavyoweza kulinda na
katiba ya nchi.
Mwezeshaji, Mwandishi wa Habari, Mwanasheria, msomi na mjumbe wa Bunge la Katiba Ali Uki akizungumza kwenye warsha hiyo.
“waandishi kwa kutumia nafasi yao wanaweza kushauri kwa kurekebishwa
baadhi ya sheria, vifungu ili kuweza kulinda haki za binadamu nchini kwa
kupitia bunge maalum la katiba,” aliongeza.
Alisisitiza Mhe Sululu kwamba bunge la katiba halijadili kuhusu ama
serikali mbili au tatu kwa sababu kuna mambo mengi kwenye rasimu ya
katiba yakujadiliwa.
“kwa jinsi mnavyoripoti kuhusu serikali mbili ama tatu ni kama mchezo
wa kamari ya majongoo jamani katiba siyo muungano tu,” amesema.
Kwa upande, Mratibu wa Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu
(THRDC), Onesmo olengurumwa amesema ingawaje kwenye rasimu ya katiba
hawajatambua watetezi wa haki za binadamu bali wataendelea kushauriana
na wajumbe kupata mwafaka wa jambo hilo.
Meza kuu, Ndg. Onesmo Olengurumwa akiwa na Mgeni rasmi Samia Suluhu Hassani kwenye warsha hiyo.
“Rasimu ya katiba haijatambua mahali popote nafasi ya mashirika
yasiyo ya kiserikali yanayotetea haki mbali mbali za raia kama
zilivyoanishwa kikatiba,” amesema
Olengurumwa aliongeza kwamba rasimu ya katiba pia haijatambua
wasaidizi wa kisheria wakujitolea (Paralegal) ambao wanatoa msaada
mkubwa kisheria kwenye ngazi za vijijini.
Amesema ni muhimu kwa watanzania kuendelea kupanua mjadala wa katiba
ili misingi ya haki za binadamu iingie kwenye mifumo ya utetezi wa haki
za binadamu nchini.
Olengurumwa amesema waandishi wa habari kama vile watetezi wa haki za
binadamu maisha yao lazima yalindwe na kutetewa na katiba ya nchi ili
kujenga mazingira mazuri ya haki za binadamu nchini.
Hivi karibuni rasimu ya pili ya Katiba ilipendekeza Muungano wa
Serikali tatu – Serikali ya Jamhuri ya Muungano, Serikali ya Mapinduzi
Zanzibar na Serikali ya Tanganyika.
Mjadala wake ulianza, ambapo wasomi walikosoa takwimu za Tume ya
Mabadiliko ya Katiba kuhusu idadi ya waliotoa maoni, kuwa zimetumika
kuupotosha umma.
wahadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Sabato Nyamsenda na
Bashiru Ally wakati wakizungumza katika kipindi cha Je, Tutafika?
kinachorushwa na Channel Ten hivi karibuni.
Baadhi ya washiriki wa warsha hiyo waandishi na wahariri kutoka vyombo mbalimbali nchini.
Nyamsenda amesema ukweli wa takwimu hizo uko kwenye ripoti ya Tume
hiyo, ambayo haipatikani kwa urahisi huku watu wakiishia tu kusoma tu
rasimu ambayo haielezi majukumu waliyopewa, mahali walipopita, idadi ya
wananchi na maoni yao.
Takwimu za Tume
Akifafanua zaidi, Nyamsenda anasema takwimu zinazotajwa kwamba
asilimia 61 ya Watanzania Bara wanataka Serikali tatu, asilimia 60 ya
Wazanzibari wanataka Serikali ya Mkataba si za kweli.
“Tume ya Warioba imetoa takwimu kuwa, watu waliotoa maoni kwa jumla
ni 333,537. Kati yao, waliogusia Muungano ni 77,000, kwa hiyo 256,537
hawakugusia Muungano,” anasema na kuongeza:
“Ukiwagawanya katika Bara utakuta ni watu wapatao 36,000 na Visiwani
watu 38,000. Kati ya waliozungumzia muungano. Kwa Zanzibar watu 19,000
hawakugusia muundo na watu 10,400 ndiyo waligusia Muungano wa Mkataba.”
Anaendelea kufafanua: “Waliozungumzia Serikali mbili ni 6,460 sawa na
asilimia 34. Kwa hiyo ni wachache kuliko waliozungumzia Serikali ya
Mkataba ambao nao ni wachache kuliko wale ambao hawakugusia kabisa suala
la muungano. Ni sawa na tone la maji katika bahari,” amesema.
Benedict Ishabakaki, Afisa Usalama wa Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu akishiriki mkutano huo.
Anaendelea kufafanua kuwa waliotoa maoni kuhusu Serikali ya Mkataba na Serikali tatu, ni wachache huku wengi wakiwa Bara.
“Kama jumla ya watu waliotoa maoni ya Katiba ni 333,537, huwezi
ukachukua watu 16,000 waliotaka Serikali tatu ukawaziba wengi ambao
hawakutaka,” anasema na kuongeza:
“Ukijumlisha watu wanaotaka Serikali moja na mbili ambao ni 16,475,
utaona ni wengi kuliko wanaotaka Serikali tatu ambao ni 16,470.”
Anasema watu hao wakiwekwa katika kundi ambalo halikugusia kabisa muundo wa muungano, ni watu 287,537 sawa na asilimia 86.
Mgeni rasmi akiwa katika picha ya pamoja na washiriki wa warsha hiyo ya siku moja.