Mhandisi wa Ujenzi kutoka Shirika la Mafuta Tanzania (TPDC), Mhandisi
Mwita Yagela (Kulia) akiwaonesha michoro ya ujenzi wa kiwanda cha kuchakata
gesi Timu ya Ukaguzi wa Miradi ya
Maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango ilipotembelea eneo la ujenzi
huo, Madimba, mkoani Mtwara. Wanaotazama ni wakaguzi hao, kutoka kushoto ni
Prof. Longinus Rutasitara, Bibi Salome Kingdom, Bibi Florence Mwanri na Bw.
Jordan Matonya.
Timu ya Ukaguzi wa Miradi ya Maendeleo kutoka Ofisi ya Rais ikijionea maendeleo
ya ujenzi wa kiwanda cha kuchakata gesi kilichopo Madimba, mkoani Mtwara.
Vongozi wa Timu ya Ukaguzi
wa Miradi ya Maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango, Prof.
Longinus Rutasitara (Kushoto) na Bibi Florence Mwanri (Kulia)
wakiangalia moja ya bomba la kusafirishia gesi. Bomba moja lina uzito wa
tani tano na urefu wa mita 11. Mpaka sasa jumla ya kilomita 350 kati ya
kilomita 492 zimeshatandazwa.
Mhandisi wa Ujenzi kutoka Shirika la Mafuta Tanzania (TPDC), Mhandisi
Mwita Yagela (Kulia) akiwaonesha mabomba ya
kusafirishia gesi Timu ya Ukaguzi wa Miradi ya Maendeleo kutoka Ofisi ya
Rais, Tume ya Mipango ilipotembelea baadhi ya maeneo yanakopita mabomba hayo. Mpaka sasa jumla ya kilomita 350 kati ya kilomita
492 zimeshatandazwa.
Mafundi wakiendelea na ujenzi wa makazi ya wafanyakazi katika kiwanda
cha kuchakata gesi kilichopo Madimba, mkoani Mtwara.
============ ==========
Na Saidi Mkabakuli
Maendeleo
ya ujenzi wa bomba la gesi kutoka Mtwara hadi Dar es Salaam unatarajiwa
kukamilika mwishoni mwa mwezi Julai mwaka huu kufuatia kuendelea vyema
kasi ya kundaza bomba hilo.
Wakizungumza
na wakaguzi wa miradi ya maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya
Mipango, Wahandisi wa Ujenzi kutoka Shirika la Mafuta Tanzania (TPDC),
Mhandisi Mwita Yagela na Mhandisi Omary Kitiku wamesema kuwa kasi ya
sasa ya ujenzi wa kiwanda cha kuchakata gesi kilichopo kijiji cha
Madimba, mkoani Mtwara inatia moyo na hivyo kuashiria kukamilika kwa
mchakato huo kwa wakati.
“Mpaka
sasa jumla ya kilomita 350 kati ya kilomita 492 za bomba la gesi kutoka
Mtwara hadi Dar es Salaam zimeshatandazwa hali inayokwenda sambamba na
mpangokazi wa ujenzi wa kiwanda hiki,” alisema Mhandisi Yagela. Kwa
mujibu wa Mpangokazi wa ujenzi wa kiwanda hiko hadi kufikia mwisho wa
Julai kiwanda kinatakiwa kukamilika, na mpaka sasa, makazi ya
wafanyakazi imekamilika.
Akizungumza
wakati wa ukaguzi huo, Mmoja wa viongozi wa Timu ya Ukaguzi wa Miradi
ya Maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango, Bibi Florence Mwanri
alisema kwamba kukamilika kwa bomba hilo kunatoa mwanya wa kukamilika
kwa wakati uzalishaji wa umeme katika vituo vya Kinyerezi, jijini Dar es
Salaam.
“Kukamilika
kwa bomba hili kunatoa fursa ya kwa Mradi wa kuzalisha umeme kiasi cha
Megawati 150 na Megawati 240 kwa kutumia gesi asilia vilivyopo
Kinyerezi, jijini Dar es Salaam,” alisema Bibi Mwanri.
Kwa
mujibu wa Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Miaka Mitano (2011/12 -
2015/16), Miundombinu ni kipaumbele cha kwanza, hasa uwekezaji mkubwa
katika miundombinu ya nishati ambapo nguvu kubwa imewekwa katika
uwekezaji wa miundombinu ya nishati ambapo utekelezaji wa ujenzi wa
bomba la gesi Mtwara hadi Dar es Salaam unafanywa sambamba na ujenzi wa
mitambo miwili ya kuzalisha umeme kwa kutumia gesi katika eneo la
Kinyerezi Dar es Salaam. Serikali imeandaa Mpango wa Maendeleo wa Miaka
Mitano (2011/12 -2015/16) wa kutekeleza Dira ya Taifa ya Maendeleo
2025.
Lengo
kuu la Mpango huu ni kufungulia fursa za ukuaji uchumi wa nchi ili
kuweka misingi ya ukuaji mpana wa uchumi na unaolenga watu walio
masikini zaidi. Mpango
wa Kwanza wa Maendeleo wa Miaka Mitano unawianisha katika mfumo mmoja
wa mipango mbalimbali ya maendeleo ya kitaifa ili kutoa mwongozo wa
utekelezaji na kuipa Serikali fursa na mfumo rasmi wa ufuatiliaji na
tathmini wa miradi ya maendeleo kitaifa. Lengo la Dira ni kuibadili
Tanzania kuwa nchi ya uchumi wa kati ifikapo mwaka 2025.