KaTtibu
Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akipata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi
wa Maji wa MCAT (Millenium Challenge Acount Tanzania,Bwana William
Christian kuhusianana namna maji yanavyokusanywa na kusambazwa maeneo
mbalimbali ya Mkoa wa Pwani na Jiji la Dar,kati ni Mkuu wa Mkoa wa
Dar,Mh.Mecky Sadicky akisikiliza.
KaTtibu
Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akiwaongoza viongozi wa CCM Wilaya ya
Kinondoni kutembelea mitambo mipya baada ya upanuzi wa mitambo ya maji
ya Ruvu Chini, wilayani Bagamoyo, kufanyika. Ujenzi wa mitambo hiyo
umegharimu sh. Trilioni 1.6. Mradi huo unaotarajia kukamilika mwaka huu
utapunguza kwa kiasi kikubwa tatizo la maji katika Mkoa wa Pwani na Dar
es Salaam. Kinana amemaliza ziara yake jijini Dar,wilayani
Kinondoni pia kwa kutembelea kituo cha mabasi ya mjini kilichopo sinza
na kufungua tawi jipya la vijana wakereketwa Kawe.
Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akiendelea kupata Maelezo kutoka kwa kutoka
kwa Mkurugenzi wa Maji wa MCAT (Millenium Challenge Acount
Tanzania,Bwana William Christian,juu ya mitambo hiyo mipya ya kuchujia
maji.Ndugu Kinana alieleza kuwa ameridhishwa na namna ya kazi ya upanuzi
wa mitambo mipya ya maji Ruvu chini inavyoendelea,ameeleza kuwa kazi
hiyo ya upanuzi ikikamilika basi jiji la Dar na maeneo mengine
mbalimbali tatizo la maji litapungua kwa asilimia kubwa.
Ndugu
Kinana na Ujumbe wake wa CCM kutoka Wilaya ya Kinondoni wakiangalia
sehemu ya kuchanganyia dawa za maji kabla ya kusambazwa kwa matumizi
mbalimbali.
upanuzi wa mitambo ya maji ya Ruvu Chini, wilayani Bagamoyo, ukiendelea.
KaTtibu
Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana pamoja na viongozi wa CCM Wilaya ya
Kinondoni wakipata maelezo mafupi kuhusiana na usambazaji wa maji maeneo
mbalimbali sambamba na namna ya upanuzi wa mitambo mipya ya maji ya
Ruvu Chini, wilayani Bagamoyo, a Ujenzi wa mitambo hiyo umegharimu sh.
Trilioni 1.6. Mradi huo unaotarajia kukamilika mwaka huu utapunguza kwa
kiasi kikubwa tatizo la maji katika Mkoa wa Pwani na Dar es Salaam.