Jarida la Washington Post nchini Marekani limeripoti kwamba askari
watatu ambao ni walinzi wa president wameachishwa kazi kwa muda na
kurudishwa nyumbani ili uchunguzi ufanyike.
Askari mmoja kati ya hao alikutwa amelewa pombe chakari kwenye hoteli
moja huko Amsterdam ambapo Obama alienda kwa ajili ya mkutano wa mambo
ya Nuclear.
Msemaji wa idara ya upelelezi Marekani alikataa kutoa taarifa zaidi
kuhusu tukio hilo ingawa alisisitiza kuwa watatu hao wameachishwa kazi
kwa muda huku uchunguzi ukiendelea.
Mwaka 2013 majasusi wawili waliondolewa katika kikosi cha ulinzi cha
Rais Obama kufuatia tuhuma za kuhusika na kashfa ya ngono na utovu wa
nidhamu.
Mwaka 2012 majasusi kadhaa waliachishwa kazi kufuatia madai kuwa walikodi makahaba walipokuwa mjini Cartagena Colombia.