Katibu
Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akizungumza na Wajasiliamali-VICOBA mbalimbali
katika mkutano uliofanyika mapema leo asubuhi ndani ya ukumbi wa Kata
ya 15,katika Wilaya ya Temeke.Kinana aliwapongeza VICOBA hao kwa kuchapa
kazi nzuri na kuwa waaminifu katika mazingira yao ya kufanya kazi.Aidha
amewataka akina mama na vijana mbalimbali kutobweteka na badala yake
wajitume kufanya kazi,katika suala zima la kujipatia maendeleo yao
sambamba na kujikwamua na Umaskini.Ndugu Kinana amefanya ziara yake leo
ya siku moja ndani ya Wilaya ya Temeke,ikiwa na lengo la Kuimarisha Uhai
wa Chama hicho na kuhamaisha utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya mwaka
2010.
Mbunge
wa Jimbo la Temeke,Abbas Mtemvu akielezea namna alivyoweza
kuwakutanisha watu wa kada mbalimbali katika kuunda VICOBA kwa ajili ya
Maendeleo yao,katika Wilaya ya Temeke mapema leo wakati wa mkutano
uliofanyika ndani ya ukumbi wa Kata ya 15,Mbele ya Katibu Mkuu wa
CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana alipokutana na VICOBA hao alipokuwa kwenye
ziara yake ya siku moja wilayani humo.
Wana-VICOBA wakifuatilia mkutano
Meneja
Mradi wa kiwanda cha kuzalisha gesi kilichopo kata ya Mtoni,Bwa.Richard
Matari akifafanua jambo mbele ya Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana
alipotembelea mradi huo na kujionea hali halisi ya eneo hilo.
Katibu
Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akipata maelezo ya mradi huo wa kuzalisha gesi
na changamoto zake,Kiwanda hicho mpaka sasa hakifanyi kazi kutokanana
kukumbwa na changamoto mbali mbali na kupelekea kusimama kutofanya kazi
mpaka sasa.
Katibu
Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana pamoja na Mkuu wa Mkoa,Mh.Meck Sadicky
wakikagua mitambo ya kuzalisha gesi inayotokana na taka taka,kilicho
Mtoni,wilayani Temeke.Kinana yuko ziarani wilayani humo kwa siku moja.
Mbunge
wa Jimbo la Temeke,Abbas Mtevu akizungumza jambo na Mkuu wa
Mkoa,Mh.Meck Sadicky nje ya ofisi za CCM,wilaya ya Temeke mapema leo
asubuhi wakati Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana alipoanza ziara yake
wilayani humo.
Katibu
Mkuu wa CCM,akiwasili kwenye ofisi za CCM,wilaya ya Temeke mapema
leo,ambapo alikutana na kamati ya siasa ya wilaya na kupewa taarifa
kamili ya hali ya kisiasa ya wilaya hiyo.
Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akipunga mkono kwa wananchi waliokuwa pembeni (hawaonekani pichani) mapema leo asubuhi.
Katibu
Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana na Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Dar,Ramadhan
Madabiba wakiwa ndani ya bajaji (hawaonekani),wakielekea kwenye mkutano
mfupi wa kukutana na wajasiliamali-VICOBA,ndani ya ukumbi wa Kata ya
15,wilayani Temeke.Kinana yupo wilayani humo kwa ziara ya siku moja.
Baadhi
ya akina mama mbalimbali waliojiunga kwenye VICOBA wakishangilia
jambo,wakati wa mkutano mfupi uliowakutanisha na Katibu Mkuu wa
CCM,Ndugu Kinana,ambaye alizungumza nao na kuwatia moyo katika juhudi
zao mbalimbali za kupambana na kujikwamua na lindi la umaskini.Kinana
aliwaasa VICOBA hao kutobweteka na badala yake wafanye kazi kwa bidii na
kujitegemea bila ya kusubiri ajira.
Mkutano ukiendelea
Mwakilishi
wa VICOBA wilaya ya Temeke,Mariam Temela akisoma hotuba yake fupi mbele
ya Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana mapema leo asubuhi katika Wilaya ya
Temeke wakati wa mkutano uliofanyika ndani ya ukumbi wa Kata ya 15
uliojumuisha VICOBA mbalimbali (hawapo pichani).
Mwakilishi
wa VICOBA wilaya ya Temeke,Mariam Temela akikabidhi hotuba yake fupi
aliyoisoma mbele ya Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana mapema leo asubuhi
katika Wilaya ya Temeke wakati wa mkutano uliofanyika ndani ya ukumbi
wa Kata ya 15 uliojumuisha VICOBA mbalimbali.