Kaimu mkuu wa shule ya sekondari Unyahati jimbo la Singida, Mboya David akiwa ofisini kwake akitekeleza majukumu yake.
Meza ya mkuu wa shule ya sekondari ya Unyahati jimbo la Singida mashariki linaloshikiliwa na CHADEMA.
Kutokana
na ofisi ya mkuu wa shule ya sekondari ya Unyahati jimbo la Singida
mashariki kutokuwa na kabati za kutunzia nyaraka imelazimika kutumia
viti vya plastiki kutunza nyaraka mbalimbali.
Mwalimu
Mboya David kaimu mkuu wa shule ya sekondari ya kata Unyahati jimbo la
Singida mashariki ambalo mbunge wake ni Tundu Lissu aliyejipatia
umaarufu kwa hoja zake bugeni, akikagua choo cha nyasi chenye matundu
nane kinachotumiwa na wanafunzi wavulana 173 wa shule hiyo.
Wanafunzi
wa kidato cha kwanza shule ya sekondari Unyahati jimbo la Singida
mashariki,wanaketi kwenye viti vya plastiki na kuandikia kwenye mapaja
yao kutokana na kukosa madawati.(Picha na Nathaniel Limu).
.Shule za sekondari jimboni kwake zipo hoi kwa madawati na vyoo
Na Nathaniel Limu, Ikungi
SHULE
ya sekondari ya Unyahati iliyopo kijijini kwa mbunge wa jimbo la
Singida Mashariki (CHADEMA),Tundu Lissu inakabiliwa na changamoto
nyingi, ikiwemo ya uhaba mkubwa wa vyoo hali inayochangia wanafunzi
kutumia choo cha nyasi.
Kaimu
mkuu wa shule hiyo, Mbaya David amesema kuwa kutokana na wazazi/walezi
wa jimbo hilo kuwa kwenye mgomo wa kuchangia wala kushiriki miradi yao
ya maendeleo mbalimbali ikiwemo ya sekta ya elimu,hali hiyo imechangia
mwaka jana walimu wa shule hiyo na wanafunzi kuchimba choo ambacho
wakati wa masika, kilidumbukia kutokana na kuwa chini ya kiwango.
“Jimbo
hili ukitamka jambo la michango au watu kushiriki utekelezaji wa
miradi, huwezi kueleweka.Wazazi/walezi wameishaambiwa kuwa serikali ina
fedha nyingi ya kugharamia miradi yote na wao kama wananchi, hawahusika
kabisa na jukumu hilo”amesema.
Kwa hali hiyo, amesema ili shule isije ikafungwa kwa kukosa choo, shule imeamua ijenge choo cha muda ambacho ni cha nyasi.
David
amesema pamoja na changamoto ya choo zipo zingine ikiwemo ya wanafunzi
wa kidato cha kwanza kutumia viti vya plastiki darasani na hali hiyo
inachangia waandikie juu ya mapaja yao.
Kaimu
mkuu huyo wa shule, alitaja changamoto zingine kuwa shule hiyo haina
kabisa nyumba za walimu kitendo kinachochangia wapange katika kijiji cha
Ikungi kilichopo umbali wa kilomita nne. Hali hiyo inachangia mwalimu
kutembea kilomita nane kwa siku kwenda shuleni.
“Hapa
kwetu hatuna jengo la utawala jambo linalosababisha tubadilishe
matumizi ya vyumba viwili vya madarasa na kuwa ofisi za
walimu.Tunakabiliwa na upungufu mkumbwa wa samani ikiwemo makabati
kitendo kinachotulazimisha kutumia viti vya plasitiki kuhifadhia nyaraka
mbalimbali”, amesema Divid.
Kuhusu
vyumba vitatu vya maabara, David amesema kuwa hali ni mbaya mno kwa
sababu hata kutenga eneo lenyewe la kujenga vyumba hivyo halijatengwa.
Kwa
mujibu wa uongozi wa shule hiyo ingawa shule hiyo imejengwa kijijini
kwa Tundu Lissu, lakini toka ianzishwe miaka saba iliyopita mbunge huyo
hajaweza kutembelea shuleni hapo.
Kwa
mujibu wa taarifa zilizopatikana shuleni hapo, hakuna ndugu wa karibu
na mbunge Tundu anayesoma shuleni hapo. Hata hivyo mbunge Tundu Lissu,
amealikwa kwenye harambee ya kuchangia maendeleo ya shule ya kijijini
kwao.
Juhudi
za kumpata Tundu aweze kuzungumzia changamoto za shule hiyo zilikwama
baada ya kumtumia ujumbe kwa njia ya simu hakujibu na alipopigiwa,
hakupokea.
Hivi
karibuni mkuu wa wilaya ya Ikungi, Manju Msambya amesema kuwa kabla ya
mwaka 2010 wakazi wa jimbo hilo walikuwa mstari wa mbele katika kujenga
shule za sekondari za kata na kata mbili zilijenga sekondari mbili.
Baada ya uchaguzi mkuu wa 2010 mambo yalibadilika baada wananchi
kukatazwa kuchangia maendeleo yao.