TUME ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imebaini kuwepo kwa hujuma katika uchaguzi mdogo wa Jimbo la Chalinze unaotarajiwa kufanyika Aprili 6, mwaka huu.
Uchaguzi
huo unafanyika baada ya nafasi hiyo kuwa wazi kutokana na kufariki kwa
aliyekuwa Mbunge wa Jimbo hilo, Saidi Bwanamdogo, aliyefariki Januari
22, mwaka huu.
Taarifa
iliyotolewa na Mwenyekiti wa Tume hiyo, Jaji Mstaafu Damian Lubuva, kwa
vyombo vya habari ilieleza kuwa Tume hiyo imekuwa ikifuatilia kampeni
za uchaguzi huo ambazo zimekuwa zikifanywa katika maeneo mbalimbali ya
jimbo hilo.
Tume
hiyo imebaini kuwa baadhi ya vyama vimekuwa vikitumia lugha za chuki na
sizizo na stahaha na hata kuhamasisha wananchi kuchukua sheria mkononi
pamoja na kutoa vitisho kwa wapigakura kwa lengo la kuwazuia wasishiriki
katika uchaguzi huo.
Tume
hiyo imekemea kwa nguvu zake zote na kulaani vitendo hivyo
vinavyofanywa na baadhi ya vyama vya siasa pamoja na wagombea bila
kuzingatia sheria, kanuni, taratibu na maadili ya uchaguzi
yaliyokubaliwa na vyama hivyo vinavyoshiriki katika uchaguzi.
Tume
inasisitiza vyama vyote vya siasa na wagombea kufanya kampeni za
kiungwana na kunadi sera za vyama vyao bila kuvunja sheria
zilizoainishwa ikiwa ni pamoja na kutokuhamasisha wananchi kujichukulia
sheria mkononi.
"Tume
inatarajia kuona kuwa kila mwananchi mwenye sifa za kupiga kura kwenye
jimbo hilo ana tumia haki yake ya kikatiba na sheria kupiga kura kwa
amani na utulivu pasipo vitisho wala kubughudhiwa,"alisema
>>Majira
>>Majira