Sisty Nyahoza Msajili masidizi ofisi ya msajili wa
vyama vya siasa akizungumza na waandhishi wa habari katika ukumbi wa
Masai Chalinze kuhusu mwenendo wa kampeni za vyama na wagombea wa
uchaguzi mdogo wa jimbo la Chalinze unaotarajiwa kufanyika Aprili 6
mwaka huu, kutoka kushoto ni Muhidini Mapayo Mwanasheria na kiongozi wa
timu ya Ofisi ya Msajili Chalinze na Erald Martin Ofisa Sheria.Sisty Nyahoza Msajili masidizi ofisi ya msajili wa
vyama vya siasa akizungumza na waandhishi wa habari katika ukumbi wa
Masai Chalinze kuhusu mwenendo wa kampeni za vyama na wagombea wa
uchaguzi mdogo wa jimbo la Chalinze, kulia ni Isaya Makoko Ofisa sheria
na kushoto ni Erald Martin pia Ofisa Sheria
…………………………………………………………………………………
1.0 UTANGULIZI
Ndugu
zangu wanahabari, awali ya yote nawashukuru sana kwa kuitikia wito wa
Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa. Natambua mna majukumu mengi ya
kuhabarisha umma, hasa katika kipindi hiki ambacho nchi yetu ipo katika
mchakato wa mabadiliko ya katiba na uchaguzi huu mdogo wa Chalinze.
Kwanza
nianze kwa kuvipongeza vyama vyote vya siasa ambavyo vimeweka wagombea
katika uchaguzi huu. Hivi sasa hapa nchini kuna vyama vya siasa ishirini
na moja (21) vyenye usajili wa kudumu na ambavyo kisheria vinastahili
kushiriki chaguzi zote, lakini vyama vya siasa vilivyofanikiwa kuweka
wagombea ni vitano (5) tu, AFP, CCM, CHADEMA, CUF na NRA. Pongezi hizi
nazitoa kwa kutambua kuwa, kushiriki uchaguzi ni gharama.
2.0 MAJUKUMU YA OFISI YA MSAJILI WA VYAMA VYA SIASA KATIKA UCHAGUZI
Kabla
ya kuwaeleza madhumuni ya kuwaita, naomba kwanza nitumie nafasi hii
kuwaeleza majukumu ya Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa katika
uchaguzi, kwani kuna wadau ambao bado hawaelewi kwa nini Ofisi ya
Msajili wa Vyama vya Siasa ipo katika jimbo la Chalinze na Ofisi hii
inafanya nini katika uchaguzi huu.
Ofisi
ya Msajili wa Vyama vya Siasa ina jukumu la kusimamia utekelezaji wa
Sheria ya Vyama vya Siasa namba 5 ya mwaka 1992 na Sheria ya Gharama za
Uchaguzi namba 7 ya mwaka 2010 katika chaguzi zote ikiwamo chaguzi ndogo
za wabunge na madiwani.
Katika
kusimamia utekelezaji wa Sheria ya Vyama vya Siasa, Ofisi ya Msajili wa
Vyama vya Siasa inafuatilia na kutoa adhabu kwa vyama vya siasa
vinavyojihusisha na vitendo vifuatavyo:-
a)
Chama ambacho wanachama na/au mashabiki wake wanajihusisha na vitendo
vya fujo, vurugu na uvunjifu wa amani wa aina yoyote ile;
b) Chama ambacho viongozi na/au wanachama wake wanatumia maneno ya matusi, kashfa na uchochezi; na
c) Chama ambacho kinatumia na/au mgombea wake anatumia mali za Serikali katika kampeni na uchaguzi.
Katika
kusimamia utekelezaji wa Sheria ya Gharama za Uchaguzi, Ofisi ya
Msajili wa Vyama vya Siasa ina jukumu la kuweka sawa uwanja wa ushindani
katika siasa, kwa kufuatilia na kupendekeza/kutoa adhabu kwa chama cha
siasa na/au mgombea anayejihusisha na masuala yafuatayo.
a)
Kutumia fedha nyingi zaidi ya kiwango kilichowekwa na Sheria katika
jimbo husika. Katika jimbo la Chalinze sheria inasema mgombea asitumie
zaidi ya shilingi milioni hamsini;