SERIKALI imewaamrisha maafisa wa polisi kuwapiga risasi na
kuwauwa washukiwa wa ujambazi waliowamiminia risasi waumini waliokuwa
kanisani siku ya Jumapili na kuwauwa watu sita huku wengine 17 wakiachwa
na mejeraha ya risasi.
Wakati huo huo polisi wametakiwa kuwauwa majambazi wanaoendelea kuhangaisha wakazi wa kaunti ya Mombasa.
Akitoa amri hiyo mwneyekiti wa
kamati ya usalama katika kaunti ya Mombasa Bw Nelson Marwa alisema
majangili na magaidi hawafai msamaha, huruma ama kupelekwa mahakamani
huku akivitaka vyombo vya usalama kukabiliana nao mara moja.
Akiongea kwneye mkutano wa kiusalama
kati ya viongozi wa makanisa yote katika kaunti hiyo kamishna huyu wa
kaunti ya Mombasa alisema wahalifu waliouwa wamunimi kanisani hawafai
kupelekwa mahakamani kwa kuua.
“Hao si watu wakutiwa mbaroni ati
kwa sababu wamejihami! Wanafaa kumalizwa papo hapo. Kwa nini wapelekwe
mahakamani ilhali wameuwa watu sita? Kuna haki gani kwa waliouwawa? Nani
atakuwa shahidi yako kortini? Nani atawafufua uliowauwa ili wawe
mashahidi wako? Lazima tuwe watu wa haki wakipatikana wauliwe maramoja”
akaagiza.
Alisema operesheni ya kuwasaka
wahalifu hao imesambazwa hadi kaunti za KIlifi na Kwale huku akionywa
kwamba wataingia hadi katika Kaya kuwasaka.
Alisema kwa sasa wamekamata
washukiwa 109 ambao wamo mikononi mwa maafisa wa polisi huku akiongeza
kuwa hata kivukio cha feri kimezungukwa na maafisa wa polisi wenye
mavazi ya sare na wale wenye mavazi ya kawaida.
“Kivukio cha Feri inayotumiwa na
maelfu ya Wakenya huko tumetuma maafisa wa polisi washike doria.
Wahalifu ambao wametorokea katika Kaya wajue tutawafuata hadi huko ndani
serikali itafanya kile liwezavyo ili wachukuliwe hatua” akasema.
Mwenyekiti wa muungano wa makanisa
Mombasa Askofu Wilred Lai alisema, “Wale ambao wanadhania watatutishia
Kanisani wajue hilo ni ndoto Mkristo hawezi kutishika na kushindwa
kwenda Kanisani. Tutaendelea kuhubiri amani na neon la Munguna
atapambana na nyinyi.”
Walisema watawasaidia familia za wendazake na walioathirika kwa shambulizi la Kanisani ikiwemo mazishi.
Bw Marwa alisema viongozi wa makanisa na misitiki wataunda kamati ambao itashughulikia maswala ya usalama.
Haya yanajiri siku moja tu baada ya
serikali ya Marekani kuapa kuisaidia nchi ya Kenya katika kukabiliana na
kupambana na ugaidi hususan katika kudhibiti mipaka ya Kenya.
Maisha
Balozi wa Marekani humu nchini
Robert Godec alisema mashambulizi yanayotekelezwa na kundi la kigaidi ya
Al Shabaab yatahujumu maisha ya wakenya.
“Tunawapa pole wale wote waliopoteza
jamaa zao katika shambulizi la Kanisa. Serikali ya Marekani inashtumu
shambulizi hilo. Serikali ya Marekani itawaunga mkono jeshi la Kenya
(KDF) ipambane na misimamo mikali wanaotekeleza mashambulizi wanafaa
kukamatwa na kushtakiwa” akasema.
Naye Gavana wa Mombasa Hassan Joho
akawarai wakazi wa eneo hilo kusimama pamoja na kutotikishwa na
shambulizi hilo huku akiapa kwamba lililofanyika halitafanyika tena.
“Hakuna mtu mwenye ruhusa yakuchukua
maisha ya mwenzake hususan mtoto mdogo ambaye hana hatia alienda
kanisani kuomba tu” akasema.
Akiongeza,” Tunataka waliotekeleza
shambulizi hilo wachukuliwe hatua hatutaki watu kupiga domo tu,
uchunguzi w akina ufanywe na haki itendeke.”
Akisisitiza kwamba, pigana na nafsi
yako! acha uhalifu, acha ulevi, swali, fanya ibada hiyo ndiyo Jihad.
Lakini hii kuleta watoto wadogowadogo kuwafundisha uhalifu kuwatia moto
waende wapigane na wengine ati jihad? hakuna Jihad sasa, hakuna, Jihad
iliisha, Jihad iliyobaki ni Jihad yako na Mungu wako wewe kama
binadamu”.
Walikuwa wakiongea kwenye halfa la kifua kikuu kaunti ya Mombasa.