MVUA YALETA SHIDA JIJINI DAR, TAZAMA PICHA HIZI

Mwavuli unaotumiwa na wafanyabiashara wadogowadogo  ukiwa umechukuliwa na maji na kutumbukia kwenye shimo eneo la stendi ya mabasi Ubungo.
         Maji yakiwa yametuama kwenye shimo stendi ya mabasi Ubungo.

Mvua iliyonyesha usiku wa kuamkia jana na leo imesababisha maafa kwenye baadhi ya maeneo ya jiji la Dar es Salaam ambapo katika mizunguko ya  kamera yetu  imenasa  eneo la nje ya stendi ya Mkoa, Ubungo maji yakiwa yamejaa kila  pande huku wafanyabiashara wadogo wanaofanyia kazi eneo hilo, miavuli yao na vitendea kazi vikisombwa na maji huku mashimo yaliyokuwa yamechibwa katika utengenezaji wa barabara yakizidi kuporomoka.

(Stori/Picha: Gladness Mallya/GPL)


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo