Na Nyemo Chilongani
STAA wa Bongo Movies, Miriam Jolwa ‘Jini Kabula’ amefunguka kuwa
amekuwa akipigiwa simu na mtu asiyemfahamu na kumtaka akafanye biashara
ya kujiuza ‘ukahaba’ nchini China.
Akizungumza na paparazi wetu, Jini Kabula alisema katika maisha yake
anaamini maisha mazuri hata Bongo yanapatikana hivyo licha ya
kutangaziwa dau la maana lakini amekataa.
“Nimekuwa nikipigiwa simu mara kwa mara na mwanamke mmoja ili niende
nchini China kujiuza lakini nimekuwa nikimkatalia, najitambua mimi
sikubali,” alisema Jini Kabula.