Waziri wa Ulinzi wa Malaysia
ambaye pia ni Kaimu waziri wa Usafirishaji, Hishammuddin Hussein
akionyesha picha zinazodaiwa kuwa mabaki ya ndege iliyopotea.
Serikali ya Malaysia imesema kuwa picha mpya za
Satelite zimeonyesha zaidi ya vifaa miamoja vinavyodhaniwa kuwa mabaki
ya ndege yake iliyotoweka zaidi ya wiki mbili zilizopita.
Hadi kufikia sasa, hakuna taarifa rasmi ya mabaki ya ndege hiyo kuonekana.
Ndege hiyo iliyokuwa na abiria 239, ilikuwa safarini kutoka Kuala Lumpur kuelekea Beijing zaidi ya wiki mbili zilizopita.
Msako uliofanywa baharini na angani, kuitafuta ndege hiyo umeanza tena katika pwani ya Australia baada mawimbi kutulia baharini.
CHANZO: BBC SWAHILI NA DAILYMAIL.