Mkuu
wa Mkoa wa Ruvuma Said Mwambungu akiwa katika daraja la Chimate ambalo
mbao zake zimeoza na kupelekea kuhatarisha usalama kwa watumiaji wa
daraja hilo katika Wialaya ya Nyasa, ambapo alitoa agizo kwa Meneja wa
TANROADS mkoani humo kubadili mbao.
Pichani aliyesimama katikati ni Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Said Mwambungu
akiwa katika daraja la kijiji cha Mbui ambacho daraja la mto Ng’ombo
limesombwa na maji na kukigawa kijiji hicho sehemu mbili, sehemu moja
ikiwa ina shule na sehemu moja kukiwa na zahanati.
Pichanini
dereva wa ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma aliyejulikana kwa jina moja
la Komba akitoa msaada wa kuwavusha watoto wa shule katika daraja la mto
Mbui ambalo ni lamuda lililotengenezwa na wananchi wenyewe wa kijiji
cha Ng’ombo.
Kuliani
Mwenyekiti wa CCM, Mh. Oddo Mwisho akiteta jambo na Mkuu wa Mkoa wa
Ruvuma Said Mwambungu kuhusiana na daraja hilo lilisombwa na maji.
Wakazi
wa kijiji cha Ng'ombo wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Said
Mwambungu ambaye hayupo pichani akiwataka wakazi hao kuwa na subira
katika ujenzi wa daraja hilo kutokana na mto huo kuwa na tabia za
kuhamahama.
JIUNGE NA EDMO BLOG SASA
Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube
Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi