Msanii
wa kundi la Mizengwe, Hemed Maliyaga (wa kwanza kulia) akisaidiana na
ndugu pamoja na mke wa Mkambala (wa tatu kushoto) kumpeleka mgonjwa
Theatre.
STORI: DEOGRATIUS MONGELA
Baada ya Mtangazaji wa Channel Salumu Mkambala kupata ajali na
kugongana na lori akiwa safarini kuelekea Morogoro sababu za ajali hiyo
zimetajwa.
Akizungumza na mwandishi wetu Hospitali ya Tumbi Kibaha, Pwani
mdogo wa mtangazaji huyo, Ramadhani Mkambala alisema kaka yake alikuwa
akielekea Morogoro na alipofika maeneo ya Vigwaza aligongana na lori
alfajiri saa 10. 30 akiwa yeye na mtu mmoja aliyempa lifti.
Hata hivyo, chanzo cha ajali hiyo kilitajwa na Ramadhani kuwa ni
kutokana na barabara ya eneo hilo kuwa na mashimo mengi hali
iliyosababisha gari la kaka yake kuhama upande wake na kulivamia lori.
“Tulipopata taarifa tulishtuka sana lakini tunashukuru Mungu kuona
kaka yangu yupo hai na amepata matibabu hapa Hospital ya Tumbi japokuwa
ameumia mikononi na miguu na kuwekewa bendeji ngumu (POP) lakini tuna
matumaini atapona na kuendelea na majukumu yake,” alisema Ramadhani.
credits: GPL