Imeelezwa
kuwa mradi wa umeme katika kata ya Tandala na vijiji vilivyopitiwa na
mradi huo Wilayani Makete Mkoani Njombe vitaanza kunufaika na mradi huo pindi
baadhi ya vifaa vya kukamilisha mradi huo vitakapowasili
Akizungumza
na Kitulo fm Meneja wa Shirika la Umeme Tanzania TANESCO Wilaya ya Makete Bw. Zebedayo
Gadau amesema tayari mradi huo uko katika hatua za mwisho na kinachosubiriwa ni
baadhi ya vifaa vya kuunganisha umeme kwenye “Service line” ambapo amesema
muda wowote vifaa hivyo vikifika watu wataingiziwa umeme majumbani
mwao
Aidha
Bw. Gadau ametoa wito kwa wakazi wa Kata ya Tandala kujitokeza kuchukua
fomu za kujiunga na huduma za kuingiziwa umeme majumbani kwani amesema mpaka
sasa ni watu 60 tu kati ya wakazi 2000 wanaishi katika Kata ya Tandala na
vijiji vilivyopitiwa na Mradi huo
Kwa
upande wake Diwani wa kata ya Tandala Mh. Eginatio Mtawa amesema pamoja na jitihada
za Serikali kupeleka umeme katika kata ya Tandala lakini bado wananchi wamekuwa
na mwitikio mdogo katika ujazaji wa fomu za kujiunga na huduma ya
kuingiziwa umeme ambapo amesema ni watu 60 tu walio jaza fomu kati ya wakazi 2000.
Hata
hivyo baadhi ya wananchi wamekuwa na mtazamo tofauti kuhusu kucheleweshwa
kwa kuunganishiwa umeme majumbani mwao kuwa ni pamoja na mambo ya kisiasa na kwamba
mradi huo wanaamini utakamilika kipindi cha kampeni za uchaguzi nasio sasa .
Na Aldo Sanga