Stori: Hamida Hassan na Shakor Jongo VIA GPL
KIJOGOO wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ amewachefua
waumini wenzake wa Kiislamu baada ya kutupia swaga za staili ya Ngololo
kwenye shughuli ya Maulidi.
Tukio hilo lililowagusa waumini hao lilitokea juzikati ambapo
kulifanyika Maulidi ya kumtoa nje mtoto wa dansa wake aitwaye Moze Lyobo
maeneo ya Mbagala, jijini Dar.
Awali watu waliokuwepo eneo hilo walifurahia uwepo wake lakini kadiri
walivyoaanza kugundua kasoro ndipo mambo yalipoanza kuharibika.
“Watu hawakumshtukia, lakini walipomkagua kwa makini na kugundua licha ya kuvaa mavazi ya Kiislamu ndani yake ana macheni ya dhahabu shingoni kitu ambacho dini hairuhusu,” kilidai chanzo baada ya mwandishi wetu kufika eneo la tukio na kukuta shughuli imeisha.
Kama hiyo haitoshi, ikaelezwa kuwa Diamond alizidi kuchafua hali ya hewa baada ya kucheza staili ya Ngololo kwenye kaswida kitu ambacho kiliwashangaza wengi.
“Mwanzo alianza vizuri lakini kadiri dufu lilivyokuwa linakolea, akawa anajisahau na kucheza Ngololo, kimsingi aliwaboa baadhi ya Waislamu waliokuwa pale,” alisema shuhuda wetu.
Hata hivyo paparazi wetu alitonywa kuwa, baada ya kucheza sana, Diamond alichoka huku jasho likimchuruzika ambapo aliamua kupumzika na kuwaacha wengine wakiendelea.