WATU wawili wanaosadikiwa kuwa majambazi, wamefariki dunia wakiwa njiani kupelekwa Hospitali ya Wilaya ya Tarime, mkoani Mara ili kupatiwa matibabu baada ya kujeruhiwa na risasi walizopigwa na wenzao.
Akizungumza
na waandishi wa habari, Kamanda wa Mkoa wa Kipolisi wa Tarime/Rorya,
Justus Kamugisha, alisema tukio hilo limetokea juzi saa 2:40 asubuhi,
katika Kitongoji cha Kokemange, Kijiji cha Nyamwaga, wilayani Tarime.
Alisema
watu hao walipigwa risasi na majambazi wenzao wakiwa njiani kuwapeleka
polisi eneo wenzao walijificha na silaha walizokuwa wakizitumia kufanya
uhalifu.
Aliwataja
waliokufa kuwa ni Wambura Sagare Orondo (26), mkazi wa Kitongoji cha
Nyaichirichiri, Kijiji cha Kitawasi ambaye alijeruhiwa vibaya tumboni na
Shabani Nyang'era 45, mkazi wa Kijiji cha Borenga, Wilaya ya Serengeti,
aliyejeruhiwa kifuani.
"Katika
tukio hili, polisi walijibu shambulio la risasi hivyo majambazi
waliojificha walifanikiwa kutoroka na kutelekeza bunduki moja aina ya G3
ambayo namba zake zimefutwa na imekatwa kitako pamoja na risasi tano
katika magazini.
"Hawa
majambazi waliofariki, walikuwa wakitafutwa muda mrefu kwa tuhuma za
unyang'anyi wa kutumia silaha, mauaji na wizi wa mifugo," alisema
Kamanda Kamugisha.
Aliongeza
kuwa, chanzo cha tukio hilo ni baada ya majambazi kutoka nchi jirani ya
Kenya, kubaini wanafuatiliwa na kuamua kujihami kwa kufyatua risasi.
Aliwaomba
wananchi waendelee kutoa taarifa kwa jeshi hilo ili watuhumiwa wa
unyang'anyi na mauaji waweze kukamatwana kufikishwa katika vyombo vya
sheria.
>>MAJIRA
>>MAJIRA