TAZAMA PICHA::MWANDISHI WA HABARI FEKI ALIVYONASWA LIVE AKITAKA KUMUIBIA MH. SHABIBY HUKO DODOMA...!

mwandishi wa habari feki aliyejitambulisha kwa jina la meshaki alijukuta kwenye wakati mgumu siku ya leo baada ya zoezi lake la kutaka kumtapeli mheshimiwa shabiby na kujifanya yeye ni mhariri wa gazeti la dira ya mtanzania,
Mwandishi wa habari feki  akiwa mikononi mwa vyombo vya dola baada ya kushtukiwa:

Mhariri huyu feki alitumia janja ya kumtumia ujumbe mfupi wa maneno mh na kujitambulisha kuwa yeye ni mhariri mkuu wa gazeti la Dira,.
lakini zoezi hilo lilikuwa ngumu kufanikiwa kwa mhariri huyo feki baada ya mheshimiwa kumshtukia na pia alikuwa anamfahamu vizuri mhariri mkuu wa gazeti hilo, Mhariri feki huyo baada ya kuona ameshtukiwa aliamua kukiri na kuomba msamaha na kudai kuwa ni ugumu wa maisha ndio umemsababishia hali hiyo, 
Kutokana hali na huruma Ya mheshimiwa shabiby aliyokuwa nayo aliamua kumsamehe na kumpatia fedha zaidi ya laki moja, Ila mhariri feki huyo anashikiwa na jeshi la polisi kwa kuadhalilisha taaluma hiyo na pia kulichafua gazeti hilo la Dira, Pia Mh Shabiby aliendelea kututonya kwamba kuna waandishi wengi ambao wanatumia janja hiyo ili kujipatia fedha na pia alituambia kwamba alishawahi kumshtukia mwandishi wa gazeti la Nipashe na baada ya kuona ameshtukiwa anaambiwa alitoka ndiki mithili ya swala na kuacha vumbi endeo hilo

Mh Shabiby


Jeshi la polisi likifanya kazi yake
Mharir feki akiwa kajificha kwa kuziba kichwa ili asipigwe picha


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo