Mvua
zilizonyesha usiku wa kuamkia jana zimesababisha injini ya treni
kutoka Stesheni kwenda Ubungo Maziwa, kuacha njia na kusababisha
mabehewa kuanguka.
Mabehewa hayo yalianguka katika eneo la Gerezani, kutokana na utelezi katika njia ya treni.
Msemaji wa Kampuni ya Reli Tanzania (TRL), Midladjy Maez alisema tukio la kuanguka kwa mabehewa hayo, lilitokea saa 11 alfajiri ya jana wakati treni hiyo ikienda kuchukua mabehewa.
Alisema usafiri wa treni wa jana jioni, ungeendelea kuwepo kama kawaida, kwani jitihada za kuyanyanyua mabehewa hayo, zingekamilika na wananchi walitakiwa wasiwe na wasiwasi.

Maeneo mengi ya jiji, yaliathiriwa na mvua za jana, hususani barabara ambazo miundombinu yake ni mibovu.
Barabara inayotoka makaburi ya Shekilango kwenda Ubungo, imeathiriwa na mvua na kusababisha magari na pikipiki kushindwa kupita, kutokana na shimo kubwa lililopo katika barabara hiyo.
Waendesha pikipiki katika eneo hilo, walilalamikia Wakala wa Barabara (TANROADS) kushindwa kutengeneza barabara hiyo, licha ya wao kutoa malalamiko muda mrefu.
“Mvua imetuharibia, tunalazimika kuweka miguu juu ya pikipiki na abiria anaweka miguu kwenye mapaja yetu ili tupite, tunateseka sana na hili shimo,” alisema mmoja wa madereva hao.